Manchester United Yamteua Erik Ten Hag kuwa bosi Mpya

[Picha: Skysports Twitter]

Mwanadishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Manchester United imemteua Erik Ten Hag kuwa bosi mpya wa kudumu wa Red devils ambaye amekuwa meneja wa tano wa kudumu wa Manchester United tangu 2013 Sir Alex Ferguson alipostaafu klabuni hapo.

Erik Ten Hag mwenye umri wa miaka 52 atarithi nafasi hiyo kutoka kwa Ralf Rangnick ambaye aliitumikia klabu hiyo kwa takriban miezi 5 na sasa Erik Ten Hag atakuwa akiinoa United kwa mkataba wa kudumu wa miaka 3 ambao utamalizika Juni 2025.

Wakati huu ambapo Hag anakwenda kuinoa United, anakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kila kona ya Old Trafford kuhusu kuifanyia marekebisho timu hiyo na hadi sasa anachukuliwa kuwa ni Messiah wa Manchester United na mashabiki wa United ambao wanaamini kwamba Erik ten Hag anaweza kurejesha ari yao ya ushindi na timu kurejea kileleni.

Erik Ten Hag amekuwa na Ajax kwa miaka 4 iliyopita na alishinda mataji ya ligi mara mbili katika msimu wa 2018-2019 na pia 2020-2021 na anatarajiwa kupata taji kwa msimu huu.

Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com

Hivi karibuni kumekuwa na minong'ono na stori zinazowahusu Wachezaji wa United kama Paul Pogba, Dean Henderson, Juan Mata, Lee Grant na Jesse Lingard ambao wametajwa kutaka kuondoka klabuni hapo na hivyo Hag sasa anatakiwa kuelekeza nguvu zake katika kufufua ari ya United ambayo imekuwa ikiendelea katika uharibifu kwa miaka 9 iliyopita

Katika kipindi cha miaka tisa tangu Sir Alex Ferguson astaafu, United walikuwa na mataji 3 pekee ambayo ni FA cup, League cup na Europa League, na sasa wako kwenye nafasi ya kukosa Champions League kutokana na matokeo duni.

United sasa United wamejihakikishia kitita cha Euro milioni 200 kwa ajili ya kusajili wachezaji wapya wa timu hiyo, Harry Kane anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji ambao United inawawinda ili kuboresha uchezaji wake.

Leave your comment