Harmonize Azungumzia Madai Kuwa Anabifu na Jux na Darassa

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bosi wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize amefunguka kuwa hana ugomvi wowote na wasanii Jux pamoja na rapa Darassa kutoka CMG.

Pakua Nyimbo Zake Jux Bila Malipo Kwenye Mdundo

Kauli hii kutoka kwa Harmonize inakuja siku chache baada ya Jux na Darassa kulalamika kuwa Harmonize aliwahusisha kwenye orodha ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha lake la Afro East Carnival ingawa makubaliano baina ya Harmonize na uongozi wa Jux na Darassa bada haijakamilika.

Soma Pia: Harmonize Atangaza Wasanii Watakaotumbuiza Kwenye Tamasha Yake ya Afro East Carnival

Mara baada ya wasanii hao wawili kutoa maoni yao, Harmonize aliamua kuwatoa kwenye orodha ya wasanii watakaokuwepo kwenye tamasha hilo ambalo linatarajiwa kurindima jijini Dar Es Salaam.

Harmonize kuwatoa wasanii hao kwenye orodha imezua gumzo, huku mashabiki wengi wakishuku kuwa huenda pande hizo mbili zina mtafaruku.

Pakua Nyimbo Zake Darassa Bila Mlaipo Kwenye Mdundo

Akizungumza na wanahabari hivi karibuni, Harmonize alitanabaisha kuwa hakuna ugomvi wowote kati yake na Jux au Darassa. Aliongeza kuwa yale yanoyotendeka ni kwa sababu ya sintofahamu ya mawasiliano baina ya uongozi wake na ule wa Jux na Darassa.

"Kuna misundestanding zilikuwa kwa viongozi tu, kama mlivyosikia brother wangu Jux kulikuwa na miscommunication between management yangu na management yake. So hizo misundestandings zilitokea kwenye management na management nadhani watakaa watasolve," alizungumza Harmonize.

Aidha Harmonize aliongeza kuwa anamuheshimu sana Jux pamoja na Darassa na kwamba anatamani washiriki katika tamasha hilo la kuitwa Afro East Carnival.

"Itakuwa faraja kwangu kuona kaka zangu hawa (Jux na Darassa) wanakuwepo. Kwa mfano mtu kama alivyo Darassa tumeshirikiana kwenye wimbo, wimbo mzuri sana itakuwa ni faraja kuona kama tutaperform pale na sidhani kama nitakuwa mimi peke yangu watanzania wengine pia watafarijika kuona tunaperform kwa pamoja," alizungumza Harmonize.

Wasanii wengine bao wanatarajiwa kutumbuiza kwenye tamsha hilo ni pamoja na Barnaba, Cheed, Dulla Makabila, Moni Centrozone, Marioo, Skales kutokea Nigeria, Otile Brown kutokea Kenya na Eddy Kenzo kutokea Uganda pamoja na wengine wengi.

Leave your comment