Nyimbo Mpya: Bright Aachia ‘Ntakukumbuka’ Akimshirikisha Kala Jeremiah

[Picha: Bright Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki kutokea Tanzania Bright ameachia ngoma mpya ya kuitwa ‘Ntakukumbuka’ ambayo amemshirikisha rapa Kala Jeremiah.

Pakua Nyimbo Zake Bright Bure Kwenye Mdundo

‘Ntakukumbuka’ ni ngoma ya kwanza kwa Bright kwa mwaka huu. Mara ya mwisho kwa msanii huyu kuachia ngoma ilikuwa ni Desemba mwaka 2021 alipoachia ngoma ya ‘Mikono Juu’.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia ‘Flowers II’ EP

Kwenye ‘Ntakukumbuka’, Bright anaweka suala la mapenzi kando, na kwenye ngoma hii anavaa uhusika wa msanii mchanga ambaye ana ndoto ya kuwa msanii mkubwa. Bright anaomba msaada kutoka kwa Kala Jeremiah amsaidie kukamilisha ndoto zake.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia ‘Omoyo Remix’ Akimshirikisha Jane Misso

"Mziki mgumu brother nataka kutoka wasanii wengi mi walishanitosa yote nimejaribu hata kucheza soka mshika mawili vyote vimeniponyoka. Nasikia mziki bila kiki wala haukutoi. Napenda muziki sasa mbona unantesa nahustle sana ila sitoboi. Brother mi najua kuimba nishamfata mpaka Simba," anaimba Bright kwenye aya ya kwanza ya ngoma hii.

Kinachovutia zaidi kwenye ngoma hii hasa upande wa mashahiri ni namna ambavyo Bright ametumia watu halisi katika utunzi wake kwa kuwataja watu kama Diamond Platnumz, Harmonize, lebo ya King's Music, pamoja na matukio mengine mengi yanayotokea kwenye Bongo Fleva kwa sasa.

Ngoma hii imetayarishwa na Bear Beats huku video ikiwa imeshughulikiwa na Director Jay ambaye kufikia sasa ameshafanya kazi na Bright kwenye video tofauti tofauti kama vile ‘Mikono Juu’ pamoja na ‘Nakuja Dar’ aliyofanya Stamina.

https://www.youtube.com/watch?v=K5BWZlQU-zM&feature=youtu.be

Leave your comment

Top stories

More News