Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia ‘Omoyo Remix’ Akimshirikisha Jane Misso

[Picha: Mwananchi]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Harmonize ameachia ngoma yake mpya ya kuitwa ‘Omoyo Remix" ambayo ameshirikiana na msanii wa nyimbo za Injili Jane Misso.

‘Omoyo Remix’ ni wimbo ambao umetokana na ngoma ya zamani ya Jane Misso ambayo inaitwa ‘Omoyo’.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia ‘Flowers II’ EP

‘Omoyo’ ilitoka takriban miaka kumi nyuma na kwa kipindi hicho uliweza kufanya vizuri sana.

 Kwenye ‘Omoyo’ remix, Harmonize anaulalamikia moyo na hisia zake kwani ndizo hupelekea yeye kufanya maamuzi yasiyo na busara ikiwemo kuwa na kiburi, ulevi na kufanya anasa kitu ambacho Harmonize anajutia sana.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Bonge La Nyau Aachia EP Yake ‘Daktari Wa Mapenzi’

"Na waliposema mke wa mtu sumu moyo ukausema ninunue maziwa. Na ukanishawishi eti japo nimchumu mwisho wake nikafumaniwa. We moyo hauambiliki hautabiliki, moyo mgawa kiki na ndo maana huna rafiki," anaimba Harmonize kwenye aya pili ya ngoma hii.

 Siri ukali wa ngoma hii umefichwa haswa kwenye mdundo wake mchangamfu ambao unashawishi mtu kuamka na kuanza kucheza. Pia miluzi na vifijo vinavyosikika kila mara ndani ya mdundo huu ni kitu kingine ambacho watayarishaji wa ngoma hii wanatakiwa kupongezwa nacho.

Mtayarishaji wa muziki Dunga ndiye ameshiriki kuandaa ngoma hii, akiwa ni mojawapo ya watayarishaji bora wa muziki nchini ambaye ameshafanya kazi na wasanii wa kitambo kama Professa Jay, Mwasiti, Nakaaya, Ngwair, Noorah pamoja na Matonya.

https://www.youtube.com/watch?v=XPJnz4x_gR4

Leave your comment

Top stories