Nyimbo Mpya: Jux Aachia ‘I Love You’ Akimshirikisha Gyakie
4 February 2022
[Picha: Nyimbo Mpya]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Mwanamuziki Jux ameachia ngoma mpya ambayo ameipa jina la ‘I Love You’ akiwa amemshirikisha msanii Gyakie kutokea nchini Ghana.
Ngoma hii inakuja takriban wiki mbili tangu aachie ngoma yake ya ‘As Long As You Know’ na wengi wameshuku kuwa huenda ngoma hii ni maalum kwa ajili ya msimu huu wa Valentine.
Pakua Nyimbo za Jux Bila Malipo Kwenye Mdundo
"I Love You" ni ngoma ya mapenzi iliyonakshiwa na sauti nzuri kutoka kwa Jux ambaye ndani ya ngoma hii anamhakikishia mpenzi wake kuwa anampenda sana kiasi cha kupagawishwa na huba kutoka kwa mpenzi wake huyo.
"Cha ajabu hunishiki hunigusi. Ila moyo wangu nyang'anyang'a. Mwili wangu hauvutwi haupigwi tatizo moyo wangu unashindwa pambana. Everywhere you go you take my heart with you basi utulie mami naomba ntunzie," anaimba Jux kwenye aya ya kwanza ya kibao hiki.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu Aachia Video ya ‘Mwambieni’
Kwa upande wa Gyakie, anasikika zaidi kwenye aya ya pili ya ngoma hii akiimba kwa sauti yake nene na ya kuvutia, akitumia lugha ya kiingereza kuanzia mwanzo hadi mwisho kuonesha ni kwa namna gani alivyozama kwenye penzi zito na mwandani wake.
Ngoma hii imetayarishwa na Fox Made It mtayarishaji wa muziki ambaye aghalab hufanya kazi na Jux na kazi yake kubwa ambayo ameshatayarisha ni ‘Sina Neno’ ngoma ya Jux pia ambayo iliweza kufanya vizuri hapa nchini Tanzania.
Leave your comment