Wakazi Akosoa Waandaaji wa Tuzo za Muziki za Tanzania

[Picha: Music in Africa]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa kutokea nchini Tanzania Wakazi ameamua kutoa hisia zake za moyoni kuhusu tuzo za muziki ambazo zimetangazwa kufanyika mwezi Machi mwaka huu wa 2022.

Baada ya ukimya wa takriban miaka 7, siku chache zilizopita Baraza la Sanaa Tanzania walitangaza kuwa tuzo za muziki nchini Tanzania zimerudi na zinatarajiwa kufanyika Machi 26 mwaka 2022.

Pakua Nyimbo za Weusi Bila Malipo Kwenye Mdundo

Kufikia sasa, baraza hilo limeshatangaza kuwa tuzo hizo zina vipengele 23 na ndani yake kuna jumla ya tuzo 52.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Wakazi aliandika kuonesha kuwa kuna mapungufu kwenye vipengele vya tuzo hizo kwa kusema kuwa, mosi hakuna kipengele cha albamu bora ya mwaka kitu ambacho kwa upande wake amesema kuwa kutarudisha nyuma harakati za wasanii kwenye kuachia albamu.

"Hakuna kipengele cha album bora (LP & EP), na kwenye specific Category za Hip-hop maybe ya Mixtape Bora! Tumepambana kurudisha hadhi za album katika Miaka hii ya karibuni, ila Tuzo zimejikita kwenye ku acknowledge na kuzawadia singles tu bila album. This will set a bad precedent to artists na kuturudisha nyuma 10 years," aliandika Wakazi.

Wakazi pia alidokeza kukosekana kwa vipengele muhimu kwenye tuzo hizo kama mtumbuizaji bora wa mwaka pamoja na kukosekana kwa kipengele chochote kuhusu muziki wa Injili (gospel) ni moja kati ya udhaifu uliooneshwa kutoka kwa waandaaji.

Soma Pia: Rayvanny Atangaza Ujio wa EP ya ‘Flowers II’

Kando na Wakazi, msanii mwingine ambaye alionekana kukosoa tuzo hizo ni Dully Sykes ambaye siku chache nyuma itanabaisha kuwa hafikirii kuingia tena kwenye tuzo hizo kwa kuwa alishajitoa kwani waandaaji wa tuzo walishawahi kumyima tuzo miaka ya nyuma.

Leave your comment