Nyimbo Mpya: Cheed Aachia ‘Ndoa’

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Cheed ameachia ngoma mpya kabisa ambayo ameipa jina la ‘Ndoa’.

Wimbo huu unakuja takriban miezi mitatu tangu Cheed aachie ngoma yake ya mwisho ya kuitwa ‘Final’ ambayo pia iliweza kufanya vizuri sana kwenye mitaa mbalimbali hapa nchini Tanzania.

Soma Pia: Harmonize Amtaka Alikiba Kuburudisha Siku ya Kumposa Mpenzi Wake

Kwenye ‘Ndoa’, Cheed anaeleza namna ambavyo anampenda na kumhusudu sana mpenzi wake kiasi cha kutaka kufunga nae ndoa.

Cheed anatumia sauti yake nzuri kumhakikishia mpenzi wake kuwa hatomuacha na kutumia ujumbe kwa maadui zake kuwa hawataachana.

Ngoma hii ina maudhui ya kwenye harusi maudhui ambayo pia yanapatikana kwenye ngoma kama ‘Somo’ ya Kasim Mganga, ‘Iyena’ ya Diamond Platnumz na Rayvanny na ‘Nimwage’ ya Mrisho Mpoto na Harmonize.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Moni Centrozone Aachia EP Mpya ‘Road to Mazengo’

Ngoma hii imetayarishwa na Terriyo Monster ambaye pia amehusika kutayarisha ngoma ya Cheed ‘Final’ pamoja na ngoma ya Killy ‘Roho’.

Ngoma hii ni ya tatu kutoka kwa Cheed tangu ajiunge na Konde Gang, ngoma nyingine kutoka kwa Cheed tangu ajiunge na Konde Gang nyingine ni pamoja na ‘Wandia’ na ‘Final’.

https://www.youtube.com/watch?v=uZHIgxRzp3A

Leave your comment

Top stories

More News