Video ya Killy na Harmonize 'Ni Wewe' Yafutwa YouTube
20 January 2022
[Picha: Killy Instagram]
Mwandishi: Brian Sikulu
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Video ya wimbo wa Killy uliopewa jina la 'Ni Wewe' akimshirikisha staa wa muziki wa bongo Harmonize imefutwa kwenye mtandao wa YouTube.
Video hiyo iliyoachiwa tarehe 13 Januari, iliondolewa YouTube baada ya kushtakiwa kwa tuhuma za hatimiliki na mtu anayefahamika kama Ian Mutisya Munyithya kutoka Kenya.
Soma Pia: Killy Atangaza Ujio wa EP Yake ‘The Greenlight’
Ngoma hiyo tayari ilikuwa ishatazamwa zaidi ya mara milioni moja na ilikuwa imeshikilia nafasi ya kwanza kwenye orodha ya ngoma zinazovuma zaidi kwenye mtandao wa YouTube nchini Tanzania.
Akizungumza katika mahojiano na Rick Media, meneja wa Killy alisema kuwa timu ya Konde Music Worldwide inafuatilia suala hilo ili kuhakikisha kuwa video hiyo inarudishwa mtandaoni.
"Ni changamoto ambayo imetokea kweli, na hata sisi wenyewe imetupa hofu kujua ni nini tatizo linaloendelea huku mitandaoni. Kwa sababu mashabiki walikuwa wakisubiri sana video ya Ni Wewe ya Killy na ni wimbo ambao unafanya vizuri saa hizi. Na uko namba moja on Trending on YouTube. Ni suala ambalo bado linafuatiliwa, kuna mtu ambaye anahusika na social media pale ofisini bado analifuatilia kujua tatizo ni nini," meneja wa Killy alisema.
Soma Pia: Killy Ataja Producer Anayemkubali Zaidi Tanzania
Usimamizi wa Killy, hata hivyo, umedai kuwa haumfahamu Ian Mutisya Munyithya ambaye aliiripoti video hiyo.
Kufikia sasa, kisa kamili kilichosabibisha utata wa hatimiliki bado haujabainika. Mashabiki wa Killy wanasubiri kwa hamu mno huku wakitarajia kuwa ngoma hiyo itarudishwa mtandaoni.
Leave your comment