Vanillah Music Aliyeandika Ngoma ya 'Utu' Atoa Shukrani Kwa Alikiba

[Picha: Wikipedia]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Ngoma ya 'Utu' ni moja kati ya nyimbo zilizopata mapokezi mazuri kwenye albamu ya Alikiba ya 'Only One King'. Kufikia sasa ngoma hiyo imetazamwa takriban mara milioni moja nukta tisa kwenye mtandao wa YouTube japo imeachiwa kwenye mfumo wa audio tu.

Alikiba hivi karibuni alitangaza kuwa amemaliza kurekodi video ya ngoma hiyo na hivyo basi mashabiki waitarajie muda wowote. Msanii chipukizi Vanillah Music ambaye aliandika ngoma hiyo ametoa ujumbe wa shukrani kwa Alikiba na Producer Yogo ambaye aliusuka wimbo huo.

Soma Pia: Alikiba Adokeza Ujio wa Albamu Mpya Mwaka wa 2022

Kwenye ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Vanillah Music alikiri kuwa ngoma ya 'Utu' huenda ikawa kazi bora zaidi kutoka kwake kufikia sasa. Vile vile, msanii huyo alifichua kuwa ameandika ngoma mingi ambazo zimepata mafanikio makubwa japo wahusika wakuu walikubaliana kueka uhusika wake faragha.

"Nimekua nikitengeneza hit(Mziki) mbali mbali kwa wasanii tofauti tofauti kwa muda mrefu ila sikuwahi kupata heshima kubwa kama hii niliyopewa na @officialalikiba & @yogobeats," kipande cha chapisho hilo kilisomeka.

Soma Pia: Wasanii Kutoka Tanzania Wanaotazamwa Zaidi Kwa Mwaka 2022

"Watu wengi wamekua wakiniuliza hivi utaweza kuja kuandika tena wimbo mkubwa kama ulivyo fanya kwenye #UTU na zinginezo, jibu ni kwamba kabla ya utu nilisha fanya nyimbo nyingi kubwa ila kwakua wahusika wamefanya faragha basi na mimi sina budi kuheshim hilo," aliendeleza chapisho hilo.

Vanillah Music ameahidi mashabiki wake kufanya makubwa zaidi mwaka huu huku akiwaomba wamuunge mkono katika kazi zake.

Leave your comment