Nyimbo Mpya: Barakah The Prince Aachia Wimbo Mpya 'Marry You' [Video]

[Picha: Barakah The Prince nstagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika wa muziki wa Bongo Barakah The Prince ameachia ngoma mpya kwa jina la 'Marry You'.

Kwenye Ngoma hii, Barakah The Prince anamwaga hisia zake kwa mrembo na kumueleza kwa kiwango gani anampenda sana. Anamuomba wafunge pingu za maisha na akuwe mpenzi wake wa milele.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Lava Lava Aachia Video ya 'Ng'ari Ng'ari

"Samahani kwanza dada, jina lako nilijue, Kwangu inshalla kumekucha, ningependa unitambue, na moja dogo sana, ila kubwa kwangu mie, sorry kama nitakosa, na hisia zangu uniue, mi naitwa Barakah jina langu, muziki ndio kazi yangu, ila lipo tatizo langu, Mapenzi eeeh, nami natka familia yangu, niwe baba nyumbani kwangu, naomba uwe mwenzangu, tulijenge," Barakah The Prince anaimba katika kipande cha wimbo huo.

Audio ya wimbo huu imetayarishwa na Davy Machords kwa ushirikiano na Mr T Touchz.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ibraah Aachia Ngoma Mpya ‘Tanzania’

Mdundo wa ngoma hii unaenda sambamba na ujumbe uliomo kwenye wimbo. Barakah The Prince amejulikana sana kwa kuwa gwiji wa kuimba nyimbo zenye hisia haswaa za mapenzi.

Video ya wimbo huu imeelekezwa na Adam Juma. Video hii ina wahusika wawili tu ambao ni Barakah The Prince na mrembo ambaye anachukua uhusika wa kuwa mpenzi wake.

Ngoma hiyo imepokelewa vyema na mashabiki na kufikia sasa imetazwamwa na maelfu mtandaoni.

https://www.youtube.com/watch?v=URXBJgpitq8

Leave your comment