Nyimbo Mpya: Ibraah Aachia Ngoma Mpya ‘Tanzania’

[Picha: Classic 105]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Fundi wa muziki kutokea lebo ya Konde Gang Ibraah ameachia ngoma yake mpya kabisa aliyoipa jina la ‘Tanzania’.

Ibraah ambaye siku kadhaa zilizopita alifanya tamasha la Ibraah Homecoming kwa mafanikio makubwa anaachia ngoma hii ikiwa imeshapita wiki tatu tu tangu aachie ngoma yake ya ‘Addiction’ ambayo alifanya na Harmonize.

Soma Pia: Ibraah Apata Mafanikio Makubwa Katika Tamasha Lake la Ibraah Homecoming

Kwenye ngoma hii, Ibraah anaisifia nchi yake ya Tanzania kutokana na amani iliyokuwepo nchini pamoja na umahiri wa wa viongozi katika kuiongoza nchi ya Tanzania.

Ibraah pia anatoa pongezi na sifa kedekede kwa marais kama Julius Nyerere, John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa sasa Samia Suluhu Hassan. "

Alianza Nyerere baba akalijenga taifa letu akafata Mwinyi Mkapa wakatupenda viongozi wetu. Nae baba Kikwete hakubweteka wee alidumisha sana amani Kamleta John Pombe Magufuli Mungu akamchukua ingali twamtamani, sasa katupa mama, mama tuna imani nae," anaimba Ibraah.

Soma Pia: Ibraah Azungumzia Utata Uliotokea Konde Music Worldwide Kabla ya ‘Jipinde’ Kuachiwa

Ngoma hii imeandaliwa na kutayarishwa na Bad Number ambaye pia ameshiriki kuandaa ngoma ya ‘Muda’ kwenye EP mpya ya msanii Foby ambayo inaitwa ‘Me, Myself and I’.

Hii si mara ya kwanza kwa msanii Ibraah kutoa wimbo ambao umegusa upande wa kisiasa na viongozi.Mwezi Julai aliachia ngoma aliyoipa jina ‘Mama Samia’ ambayo ndani yake ametoa pongezi lukuki kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

https://www.youtube.com/watch?v=pJSJ4U70rAE

Leave your comment