Nyimbo Mpya: Mimi Mars Aachia EP Yake ya ‘Christmas With Mimi Mars’

[Picha: Mimi Mars Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki mashuhuri kutokea nchini Tanzania Mimi Mars hatimaye ameachia EP yake ‘Christmas with Mimi Mars’ ambayo imesheheni ngoma nne.

Kimaudhui, EP hii ni mahususi kwa ajili ya kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ambacho watu wengi huwa likizo kwa ajili ya sherehe za Christmas na mwaka mpya.

Soma Pia: Mimi Mars Ajibu Tetesi za Kutopewa Thamani Kwenye Muziki wa Bongo Fleva

Nyimbo zilizounda EP hii ni pamoja na ‘Christmas Day’, ‘Usiku wa Nuru’, ‘Falala’ pamoja na ‘Holy Night’.

 Kupitia EP hii, Mimi Mars ameweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kutokea Tanzania kuachia EP ambayo imesheheni ngoma za Christmas pekee. Mfumo huu wa kuachia EP maalum kwa ajili ya Christmas tulizoea kuuona kwa wasanii wa nje kama Ariana Grande kupitia EP yake ya mwaka 2013 ya ‘Christmas Kisses’ pamoja na ‘Sounds Of The Season’ EP ya Taylor Swift ya mwaka 2007.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ibraah Aachia Ngoma Mpya ‘Tanzania’

Aidha, hii ni EP ya pili kutoka kwa Mimi Mars kwani mwaka 2018 pia aliweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa kike kutoka Tanzania kuachia EP ambayo aliipa jina la ‘The Road EP’ yenye ngoma sita, huku akiwa ameshirikisha wasanii wawili ambao ni Kagwe Mungai pamoja na Nikki Wa Pili.

Leave your comment