Director Kenny Adhibitisha Rasmi Ujio wa Kampuni Yake Baada ya Kuondoka Zoom Extra

[Picha: Director Kenny Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwongozaji wa video za muziki Director Kenny hatimaye amedhibitisha rasmi ujio wa kampuni yake binafsi ya kutengeneza video.

Kupitia ukurasa wake wa kijamii, Director Kenny aliweka wazi kuwa kampuni hiyo ambayo imepewa jina la DK Limited tayari ishaundiwa ofisi zake.

Soma Pia: Harmonize Adokeza Ujio wa Kolabo Baina Yake na MB Dogg

Chapisho hilo ambalo pia limechukuliwa kama tangazo rasmi la Director Kenny kufanya kazi kibinafsi linatokea wakati ambapo tetesi za yeye kuondoka kampuni ya Zoom Extra zimesambaa mtandaoni.

Hapo awali, maswali yaliibuka baada ya ukurasa wa Instagram uliokuwa wa Zoom Extra kubadilishwa jina na kuitwa DK Limited.

Soma Pia: Nandy Atoa Lawama Zake kwa Waandaaji wa Tuzo za AFRIMA

Kufikia sasa Director Kenny amekimya kuhusu suala hilo. Japo bado hajafichua sababu ya yeye kuondoka kampuni ya Zoom Extra inayomilikiwa na msanii nyota Diamond Platnumz, ni wazi kuwa atendeleza kazi yake ya kuongoza video za muziki kupitia kampuni yake binafsi ya DK Limited.

Suala kubwa ambalo limesalia vinywani mwa mashabiki wengi ni iwapo kampuni ya Zoom Extra itafufuliwa baada ya kuondoka kwa Kenny, haswaa ikizingatiwa kuwa ukurasa wake wa kijamii ushabadilishwa jina na hivyo basi uwepo wake mtandaoni kufutwa.

Director Kenny alikuwa akifanya kazi pamoja na Hanscana alipokuwa Zoom Extra. Kwa sasa, Hanscana ndiye anaongoza video za muziki za wasanii wa WCB. Wawili hao ni kati ya waelekezaji wa video ambao wanaheshimika zaidi nchini Tanzania kwa kazi zao zenye ubora wa hali ya juu.

Leave your comment