Harmonize Adokeza Ujio wa Kolabo Baina Yake na MB Dogg

[Picha: The Citizen]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii nyota kutoka Tanzania Harmonize ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa lebo ya Konde Music Worldwide amedokeza ujio wa kolabo baina yake na mkongwe wa muziki wa bongo MB Dogg.

Kupitia ukarasa wake wa Instagram, Konde Boy kama ambavyo pia anafahamika, amesema kuwa angependa kufanya remix ya wimbo wa MB Dogg uuitwao ‘Mapenzi kitu gani’ ulioachiwa mwaka wa 2017.

Soma Pia: Nandy Atoa Lawama Zake kwa Waandaaji wa Tuzo za AFRIMA

Kwa mujibu wa Harmonize, wimbo huo umempendeza mpenzi wake Brianna na hivyo basi angependa kushirikiana na MB Dogg kwenye remix yake.

"Someone tell my brother MB Dogg how Brianna is going crazy with it. Lets go for remix 1000%," aliandika Harmonize kwenye Insta Story yake.

Kwenye chapisho lingine Harmonize alisifia sauti ya MB Dogg huku akisema kuwa alikuwa amejaliwa sauti ya kuvutia mno.

Soma Pia: Rayvanny Akerwa na Kukosa Kutajwa na Rais Kama Msanii Aliyeteuliwa Tuzo za AFRIMA

"Sauti ya nyuki MB DG ft Teacher studio tonight someone call my brother for me," chapisho lingine la Harmonize lilisomeka.

Ujumbe huo wa Harmonize umewachangamsha mashabiki wake haswaa ikizingatiwa kuwa MB Dogg ni mmoja kati ya wasanii waliochonga muziki wa bongo. Nyota huyo kwa siku za hivi karibuni ameonyesha ukaribu mno na wasanii wakongwe wa bongo.

Harmonize hapo awali pia alikuwa ameonyesha nia ya kufanya kazi na msanii 20% ambaye pia alikuwa jina kubwa katika enzi za zamani za bongo. Jeshi vile vile amemsaini msanii AT ambaye pia kwa enzi za kale za muziki wa bongo alivuma mno.

Leave your comment