Nyimbo Mpya: Chege Aachia Ngoma Mpya ‘Sinsima’

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Chege ameachia ngoma yake mpya ‘Sinsima’ ambayo amemshirikisha mwanamuziki anayeibuka kwa kasi kwenye muziki wa Bongo Fleva Saraphina.

Chege ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa lebo ya Unique Voice anaachia ngoma hii yenye vionjo vya Bongo Fleva ikiwa ni miezi miwili imepita tangu aachie ngoma yake ‘Kushki’.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Chidi Benz Aachia Albamu Mpya ‘Watu Wangu’

Kwenye ‘Sinsima’, Chege anavaa uhusika wa mwanaume ambaye anamsihi mpenzi wake awahi kufika kwenye hafla ambayo ameiandaa yeye na marafiki zake huku Saraphina akikoleza ujumbe wa ngoma hiyo kwa kumjibu Chege kuwa yupo njiani na apunguze wasiwasi kwani atafika.

"Ooh baba weee mwenzako niko njiani uache haraka na pupa napambana na foleni punguza panda shuka, nilivyojipodoa oooh watakodoa kodo kodo. Lishafika lisaa hapa kwenye mataa natamani kupaa nije nkubambe baby," anaimba Saraphina kwenye seheku ya pili ya ngoma hii.

Soma Pia: Diamond, Rayvannny, Harmonize na Wasanii Wengine Waliotazamwa Zaidi YouTube Tanzania Mwezi Novemba

Ngoma ya ‘Sinsima’ ni ya kuchezeka na kama umesikiliza ngoma ya ‘Nipigie’ ya kwake AT pamoja na Stara Thomas ya takribani miaka 11 nyuma, basi utafahamu kuwa kuna mfanano kiasi wa kimaudhui kati ya ngoma hizi mbili.

Mr T Touch ambaye ni mojawapo ya watayarishaji bora wa muziki Tanzania ndiye amehusika kutayarisha ngoma hii .

T Touch kufikia sasa ameshafanya kazi na wasanii wakubwa kutokea Tanzania ikiwemo Rapcha, Nay Wa Mitego, Billnass na wengineo wengi.

Leave your comment