Nyimbo Mpya: Chidi Benz Aachia Albamu Mpya ‘Watu Wangu’

[Picha: The Citizen]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Gwiji wa muziki wa Hip-hop kutokea Tanzania Chidi Benz hatimae ameachia albamu yake mpya aliyoipa jina la ‘Watu Wangu’.

Albamu ya ‘Watu Wangu’ imesheheni ngoma kumi na nane na kati ya hizo, ngoma sita zikiwemo ‘Walete’, ‘Nahamia Bar’, ‘King Of The Jungle’, na nyinginezo tayari zimeshatoka na hivyo kupelekea idadi ya ngoma ambazo hazijasikika kabisa kwenye albamu hiyo kuwa kumi na mbili.

Soma Pia: Chidi Benz Adai Mgwanyiko wa Wasanii Unaathiri Vibaya Tasnia ya Muziki Tanzania

Kwenye kazi hii ya kipekee, Chidi Benz ameamua kushirikisha wasanii tofauti tofauti kutokea dani na njee ya Tanzania kama vile Baddest 47, Scar Mkadinali, Only 1 Pablo pamoja na fundi wa muziki wa rap Brian Simba.

‘Watu Wangu’ ni albamu ya pili kutoka kwa Chidi Benz, albamu yake ya kwanza ilikuwa ni "Dsm Stand Up" ambayo ilitoka mwaka 2010.

‘Dsm Stand Up’ iliweza kufanya vizuri katika sehemu tofauti tofauti nchini Tanzania.

Soma Pia: Ibraah Apata Mafanikio Makubwa Katika Tamasha Lake la Ibraah Homecoming

Rapa Chidi Benz anaendeleza utamaduni wa wasanii wa Hiphop kutoa albamu kwani mwanamuziki Stamina, siku moja iliyopita ameachia albamu yake ya kuitwa "Paradiso" ambayo pia kwa sasa inafanya vizuri sana.

https://www.youtube.com/watch?v=fQ0cDOUqi1Y

Leave your comment