Amber Lulu Azungumzia Kufanya Kazi na Wasanii Wenye Upinzani Mkali Bongo

[Picha: Kidevu]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki maarufu kutokea nchini Tanzania Amber Lulu amefunguka kuhusu uhusiano wake na wasanii wakubwa nchini Tanzania ambao pia ni mahasimu.

Amber ni mmoja kati ya wasanii wachache ambao wamefanikiwa kufanya kazi na lebo za rekodi ambazo zinakisiwa kuwa na ugomvi mkali.

Soma Pia: Chidi Benz Adai Mgwanyiko wa Wasanii Unaathiri Vibaya Tasnia ya Muziki Tanzania

Kwa mfano, msanii huyo ambaye anafahamika kwa ngoma zake kama vile 'Una Shingapi', amefanya kazi na wasanii kutoka lebo ya WCB na Konde Music Worldwide. Hizi ni lebo ambazo zina upinzani mkubwa nchini Tanzania na mara mingi wasanii hugawanyika huku kila mmoja akiunga mkono lebo tofauti.

Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni kabla ya kutumbuiza kwenye tamasha la Ibraah Homecoming, Amber alisimulia jinsi amefaulu kufanya kazi na lebo hizo pinzani licha ya ugomvi uliopo.

Soma Pia: Ibraah Amshukuru Harmonize Kwa Kumsaidia Kufanikisha Tamasha la Ibraah Homecoming

Alisema kuwa yeye haegemei upande wowote na anakubali na kuchukulia wasanii wote kama familia na rafiki zake. Alifichua kuwa wasanii hao wote kutoka lebo pinzani wamemuunga mkono kwenye taaluma yake ya muziki, na hivyo basi anawakubali wote.

Aliongeza kuwa ugomvi kati ya lebo hizo hazimuhusu yeye kibanfsi kwa njia yoyote.

"Wote wameni support kwenye muziki wangu, kuna vitu ambavyo wao wako tofauti mimi havinihusu. Mimi WCB dam, Konde Gang dam, Alikiba dam," Amber Lulu alisema.

Amber Lulu ni mmoja kati ya wanamuziki wa kike ambao wanafanya vizuri sana kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania kwa sasa.

Leave your comment