Wimbo wa Ney Wa Mitego ‘Acha Niongee’ Wafutwa YouTube

[Picha: Ghafla]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Video ya wa wimbo wa ‘Acha Niongee’ wa mwanamuziki Ney wa Mitego umefutwa kwenye mtandao wa Youtube siku moja baada ya kuachiwa.

Kulingana na maelezo ya mtandao wa Youtube, video hiyo imefutwa kutokana na madai ya hatimiliki ambayo yamepelekwa huko Youtube na Rashidi Said Madega.

Soma Pia: Director Hanscana Adai Gharama ya Kutengeneza Muziki Imeongezeka

Uamuzi huo wa Youtube unakuja saa kadhaa baada ya mwanamuziki Bright kudai kuwa Ney Wa Mitego ameiba mdundo wa ngoma hiyo; ambayo walitakiwa kufanya pamoja lakini baadae Ney alibadilisha uamuzi na alitaka kufanya ngoma hiyo na Roma badala yake Bright.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bright aliandika "Wewe ndie tajiri unaepokonya kidogo cha masikini kuweka mifukoni mwako Mungu utalipa yote uliyoyafanya kwenye muziki wangu nadili na wewe. Huyu ni mwizi wa beat yangu ambayo nimeipiga mimi na nilimcheki nifanye nae wimbo (collaboration) akaleta tamaa huo wimbo wangu na beat yangu."

Soma Pia: Dully Sykes Ajibu Madai ya Kutumiwa Katika Vita Dhidi ya Harmonize

Kufikia sasa Nay wa Mitego hajazungumzia chochote kuhusiana na sakata hilo ambalo limepamba vichwa vya habarai nchini Tanzania.

Leave your comment