Harmonize Akamilisha Ziara Yake ya Muziki Marekani

[Picha: The Citizen]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkurugenzi mkuu wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize hatimaye amekamilisha ziara yake ya muziki nchini Marekani.

Kwa takriban miezi miwili iyopita, Harmonize alizuru mikoa tofauti Marekani na kutumbuiza katika hafla tofauti.

Soma Pia: Harmonize Aibua Maswali Baada ya Kuwa 'Unfollow' Wasanii wa Tanzania Kwenye Instagram

Harmonize aligonga vichwa vya habari baada ya kutangaza ziara yake ya muziki Marekani. Swali kuu kwa wakati huo lilikuwa iwapo ziara yake itapata mafanikio ambayo yeye alikuwa ametegemea.

Siku moja baada ya nyingine, staa huyo wa muziki alipanda katika jukwaa tofauti na kuwaburudisha mashabiki wake ambao walikuwa wamejitokeza kwenye matamasha yake.

Hapo awali, Harmonize alikuwa amesafiri na msanii kutokea lebo yake ya Konde Music Worldwide Ibraah. Ibraah, vile vile, aliweza kutumbuiza katika hafla tatu kwenye ziara hiyo.

Ibraah hata hivyo, alirudi Tanzania baada ya takriban mwezi mmoja ili aendelee na shughuli zingine za kimuziki. Alipokuwa Marekani kwenye ziara hiyo, Harmonize alitengeneza na kuitoa albamu yake ya pili ambayo aliipa jina la 'High School'.

Soma Pia: Serikali ya Tanzania Yampongeza Rayvanny Kwa Kuandikisha Historia Kwenye Tuzo za MTV EMA

Albamu hiyo kufikia sasa imepokelewa vizuri na mashabiki na hata kupata mamilioni ya wasikilizaji mtandaoni.

Nyota huyo kupita chapisho aliloliweka kwenye mtandao aliwashukuru mashabiki wake walioko Marekani waliomuunga mkono kwa ziara hiyo. Msanii huyo vile vile alichukua fursa hiyo kuipigia albamu yake kampeni.

"Thank You (USA) Promise 2b Back inshalla Stream Da Big #HIGHSCHOOL Usisikilize Stress Za Mvuta Ngada ...!!!! Ni swala La Kuangaika Na Muda tu Ukishaisha," Harmonize aliandika mtandaoni.

Leave your comment