Mocco Genius Ajibu Madai ya Mbosso, Zuchu Kuiba Wimbo wa Otile Brown

[Picha:YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mtayarishaji wa muziki kutokea nchini Tanzania Mocco Genius amekanusha madai kuwa vionjo au melody za wimbo wa ‘Baby Love’ kutoka kwa msanii Otile Brown zilitumika kwenye wimbo wa Mbosso na Zuchu ‘For Your Love’.

Kwa mujibu wa Mocco Genius, hajawahi kusikia wimbo huo kutoka kwa Otile Brown na hakuna kitu chochote alichonakili kwenye ngoma hiyo.

Soma Pia: Zuchu, Mbosso Wadaiwa Kuiga Melody ya Wimbo wa ‘Baby Love’ Kutoka Kwa Otile Brown

"Sina uhakika hata kama naufahamu wimbo wenyewe labda nishawahi kuisikia lakini sidhani kama naifaham. Huu wimbo mi sijawahi kuusikia, kiukweli kabisa siujui inawezekana ikawa ngoma kali kweli na nini lakini mi ngoma siijui," aliongea Mocco Genius.

"Mi kwenye beat sijasample chochote. Hakuna kitu chochote ambacho kimetoka kwenye wimbo wa mtu mwingine yeyote nimefanya mwenyewe kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Kwenye uandishi pia kwenye melody pia tumekaa tunafanya pamoja mwanzo mpaka mwisho," Mocco aliongezea.

 Genius ni mojawapo kati ya watayarishaji bora muziki nchini Tanzania ambaye kando na ngoma hii, pia alishiriki kuandaa ‘Ashua’ ya Zuchu akimshirikisha Mbosso.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mbosso Aachia ‘For Your Love’ Akimshirikisha Zuchu

Ngoma hio inapatikana kwenye EP yake Zuchu ya kuitwa ‘I am Zuchu’ iliyoingia sokoni mwaka 2020.

 

Leave your comment