Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Zuchu, Mbosso Wadaiwa Kuiga Melody ya Wimbo wa ‘Baby Love’ Kutoka Kwa Otile Brown
11 November 2021

[Picha: Pinterest]
Mwandishi: Brian Sikulu
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Masaa machache tu baada ya nyota wa muziki kutoka WCB Mbosso pamoja na mwenzake Zuchu kuachia wimbo wao uliopewa jina la ‘For Your Love’, madai yameibuka mtandaoni kwamba huenda mastaa hao wawili waliiga melody ya wimbo wa ‘Baby Love’ uliofanywa na Otile Brown kutoka Kenya.
Tuhuma hizo zilitoka kwa Otile Brown ambaye alionekana kuchukizwa na swala hilo.
Soma Pia: Marioo Azungumzia Tuhuma za Wasanii wa Bongo Kuiga Wimbo Wake ‘Beer Tamu’
Otile Brown kupitia ukurasa wake wa Instagram, hata hivyo, alionyesha upendo na uungaji mkono kwa wasanii hao licha ya kuhisi kukosewa. Otile Brown, vile vile, alichapisha kipande cha wimbo hiyo kama ushahidi wa madai yake.
Alisistiza kuwa kumekuwepo na mazoea ya wasanii kuiga melody kutoka kwa nyimbo zake ila kwa sababu yeye hana roho mbaya, basi hatachukua hatua yoyote.
”Punguzeni mazoea basi. Hio ni melody nzima ya baby love, if you know you know, mnabahati sina utoto na roho mbaya," chapisho la Otile Brown mtandaoni lilisomeka.
Soma Pia: Rayvanny Atangaza Ziara ya Muziki ya Msanii Wake Mpya Mac Voice
Kauli ya Otile Brown iliibua hisia tofauti miongoni mwa mashabiki. Wengine walimuunga mkono huku wengine wakitoa kauli tofauti na yake.
‘For Your Love’ imepokelewa vizuri na mashabiki na imefanikiwa kupata takriban watazamaji nusu milioni chini ya masaa ishirini na nne kwenye mtandao wa YouTube.
Mbosso na Zuchu wamesifiwa kwa astadi wao katika kutunga nyimbo za mapenzi, hivyo basi kolabo baina yao ilitabiriwa kuwa na uzito sana.
Weekly Top 10 songs

omelette4:28
Kyuma Radio and weasel ft Spice Diana4:07
ONLY YOU JESUS5:44
Kupenda nishapenda zaani3:12
CHAMPION GAL3:00
Nigina2:27
KIDUCHU2:12
Wano Wano2:15
Zabike2:50
Melody Ft Tunche the best3:20
Top stories
- Holy Boy (holyb374)
23 July
- Get New Hit Songs From Mock
23 July
- PLS GUYS SUPPORT ME
24 July


Leave your comment