Rayvanny Atangaza Ziara ya Muziki ya Msanii Wake Mpya Mac Voice

[Picha: Rayvanny YouTube]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkurugenzi mkuu wa lebo ya Next Level Music Rayvanny ametangaza ujio wa ziara ya muziki ya msanii Chipukizi Mac Voice.

Mac Voice ndiye msanii wa kwanza chini ya usimamizi wa Next Level Music na alitambulishwa rasmi takriban mwezi mmoja uliopita.

Soma Pia: Marioo Azungumzia Tuhuma za Wasanii wa Bongo Kuiga Wimbo Wake ‘Beer Tamu’

Utambulisho wake uliambatana na EP yake ya kwanza ambayo iko na jumla ya nyimbo sita. EP hiyo ambayo ilipewa jina la ‘My Voice’ ilipata mapokezi mazuri miongoni mwa mashabiki.

Baadhi ya ngoma kwenye EP hiyo zikiwemo ‘Nenda’ pamoja na ‘Tamu’ zimetazamwa zaidi ya mara milioni moja kwenye mtandao wa YouTube.

Baada ya kuachia EP ya ‘My Voice’ Mac Voice alifanya ziara katika vyombo vya habari. Kwenye ziara hiyo Mac Voice alifanya mahojiano ambayo yaliwapa mashabiki wake fursa ya kumjua kiundani kama msanii.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mbosso, Zuchu Waachia Video ya ‘For Your Love’

Rayvanny ametangaza hatua ifuatayo katika safari ya msanii Mac Voice ambayo ni ziara ya muziki. Japo umekuwa muda mfupi tangu kutambulishwa kwake, Mac Voice tayari anaonekana kashapanda ngazi kwenye tasnia ya muziki na jina lake lazidi kupata uziongezaa heshima.

Bosi huyo wa Next Level Music Rayvanny hata hivyo hakufichua habari zaidi kuhusu ziara hiyo haswaa ratiba na sehemu ambazo Mac Voice atazuru.

Kwa sasa Mac Voice pamoja na mashabaki wake wanazidi kusheherekea uteuzi wake kwenye tuzo za AEAUSA 2021.

Leave your comment