Nyimbo Mpya: Mbosso, Zuchu Waachia Video ya ‘For Your Love’

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Mbosso hatimaye ameachia video ya wimbo wake wa ‘For Your Love" ambao amemshirikisha mwanadada Zuchu.

Ngoma ya ‘For Your Love’ ilipita kwenye mikono ya mtayarishaji Mocco Genius na ilitoka siku tano zilizopita na tangu kuachiwa kwake imekuwa ni moja kati ya ngoma pendwa kwa mashabiki wa ndani na nje ya Tanzania.

Soma Pia: Rayvanny Kutumbuiza Kwenye Tuzo za MTV EMA Akiwa na Maluma

Kama kawaida ya Mbosso, ubunifu ni moja kati ya vitu ambavyo vimefanya video ya ‘For Your Love’ iwe ni bora sana ambapo ndani ya video hiyo Mbosso na Zuchu wanaonekana pamoja na wenzi wao kwenye mazingira tofauti tofauti ya kuvutia wakiwa kwenye mikao mbalimbali ya kimahaba.

Kilichovutia zaidi kwenye video ni namna ambavyo watayarishaji wa video hii wametumia vifaa vya kawaida kabisa kama runinga kutengeneza mandhari mazuri ya video ambayo bila shaka yatamfanya mtazamaji kuitazama video hii bila kuchoka.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Video ya Ngoma Yake ‘Baila’

Tofauti kabisa na ambavyo tumemzoea Mbosso kufanya kazi na Director Kenny, video hii imeongozwa na Slow Man Films ambayo ni kampuni ya utayarishaji video kutokea Afrika Kusini.

Kufikia sasa, Mbosso amekuwa ni msanii wa kwanza kutokea Tanzania kufanya kazi na Director huyo kutokea Afrika Kusini.

‘For Your Love’ ni video ya kwanza kutoka kwa Mbosso ndani ya miezi mitatu kwani mara ya mwisho kwa msanii huyo kuachia video ilikuwa ni mwezi Agosti mwaka huu.

https://www.youtube.com/watch?v=3GHmlVDSRPA

Leave your comment