Linex Azungumzia Madai ya Utofauti Baina Yake na Darassa

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki maarufu kutoka Tanzania Linex amekanusha madai ya uwepo wa utofauti baina yake na rapa mwenye heshima kubwa Darassa.

Madai ya uhasama yaliibuka muda mfupi baada ya wawili hao kushirikiana kwenye ngoma iliyopewa jina la ‘Sina Cha Kupoteza’.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Linex Aachia EP Mpya ‘Tatu za Mjeda’

Ngoma ya ‘Sina Cha Kupoteza’ ambayo imetayarishwa chini ya Mr. T Touch inapatikana katika EP ya LInex ambayo imepewa jina la ‘Tatu Za Mjeda’.

Kilichozua madai hayo ni ukosefu wa Darassa katika kuichapisha ngoma hiyo kwenye mitandao ya kijamii wala kupiga kampeni ya kuiuza kwa mashabiki.

Wakati ambapo Linex alikuwa akifanya mahojiano na Wasafi TV, Darassa alikuwa bado hajachapisha ngoma hiyo mtandaoni, na hivyo basi kuibua maswali miongoni mwa mashabiki.

Linex ambaye ndiye mmiliki wa ngoma hiyo, alimtetea Darassa kwa kusema kuwa mwenzake alibanwa na shughuli zake za kibinafsi. Alieleza kuwa hakuna uhasama wowote baina yake na Darrassa.

Soma Pia: Rayvanny Aweka Rekodi Baada ya Kutumbuiza Kwenye Tuzo za MTV EMA

Aidha, alimsifu Darassa kama msanii ambaye alimshika mkono na kumsaidia kimuziki. Linex alisema kuwa hana shaka kuwa Darassa atamsaidia katika kuuza muziki wake kwani wao pia na marafiki wa karibu mno.

 "Yeye ni mwanaume ana majukumu, wote kila mtu ana majukumu yake binafsi. Akanipigia simu toka jana usiku kuwa ana emergency kwamba hataweza kuzunguka na mimi... then tutafanya maybe next time sehemu zingine ambazo hatukufika na vitu kama hiyo," Linex alieleza.

Muda mfupi baada ya mahojiano hayo Darassa alichapisha kipande cha wimbo huo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusindikiza chapisho hilo na mistari kutoka kwa ngoma hiyo. "Nikienda Home Mama Mmmmh You Not Doing Better, Mapenzi Yanakuchakaza Au Ndio Kusaka Hela," Darassa aliandika mtandaoni.

Leave your comment