Lava Lava Adhibitisha Ujio wa Kolabo Baina yake na Mbuzi Gang

[Picha: Lava Lava Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki wa bongo Lava Lava amedhibitisha ujio wa kolabo baina yake na kundi la Mbuzi Gang kutoka nchini Kenya.

Kwa sasa Lava Lava yupo nchini Kenya ambako anajihusisha na kazi tofauti za kimuziki ikiwemo utengenezaji wa albamu yake.

Soma Pia: Rayvanny Atangaza Ziara ya Muziki ya Msanii Wake Mpya Mac Voice

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lava Lava alilisifu kundi la Mbuzi Gang kwa ustadi wao katika kuimba nyimbo za Gengetone.

Vile vile alitoa kauli yake kuhusu mtindo huo ambao alisema unatumia lugha ya Sheng, ambayo ni ngumu kuielewa. Kwa mujibu wa Lava Lava, japo lugha ya Sheng imempiga chenga kidogo, bado atatoa kolabo na kundi hilo.

Aliendelea kwa kusema kuwa kolabo hiyo ambayo imepewa jina la ‘Ushasema’ itakuwa kali sana na hivyo basi mashabiki wake wasubiri kwa hamu.

Aidha, Lava Lava aliulinganisho mtindo wa Gengetone kutoka Kenya na mtindo wa muziki wa Singeli kutoka Tanzania.

"Hawa Jamaa Unaowaona Hapa Wanaitwa Mbuzi Gang Hawa Jamaa Bhana Kwauku Nairobi Ndokama Watu Hatari Sana Street Yani Kwauko kwetu Mziki Wanaofanya nikama Singeli Zinavyohit Mtaani Kwanza Wanaimba Lugha Sizizoeleweka Wanaita Sheng Sasa Nimewavagaa Subiri Uone," mtandaoni lilisomeka.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Professa Jay Aachia ‘Shikilia’ Akiwashirikisha Maua Sama na Young Lunya

Lava Lava hapo awali kupitia mahojiano na mwanahabari wa Kenya Presenter Ali, aliweka wazi kuwa hayuko Kenya kwa ziara ya muziki bali kwa kolabo na wasanii wa Kenya katika nyimbo zitakazokuwepo kwenye albamu yake.

Leave your comment