Nyimbo Mpya: Abdukiba Aachia ‘Hainogi’ Akimshirikisha Alikiba

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea Kings Music Records Abdukiba ameachia ngoma yake mpya inayoitwa ‘Hainogi’ ambayo amemshirikisha Alikiba.

Ngoma ya ‘Hainogi’ imebeba wazo la tofauti ambapo Abdu Kiba anaimba kuhusu vitu ambavyo mara nyingi hutokea kwa pamoja, na ikitokea kimoja kimeondoka basi hicho kilichobakia kinakuwa hakinogi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mbosso, Zuchu Waachia Video ya ‘For Your Love’

"Ona Simba bila Yanga Hainogi, mchawi bila mganga hainogi, mchepuko bila danga hainogi, mjanga bila mshamba hainogi" anaimba Abdukiba kwenye kiitikio.

Alikiba anapokea kijiti kwenye aya ya pili ya ngoma hii akiimba "Na tukiwa na vibe hatunaga aibu, walokuja na abaya wamevua hijabu naona maajabu sasa twende club madenti wanadate mpaka na vibabuu".

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Video ya Ngoma Yake ‘Baila’

Ngoma hii ni ya kuchezeka na ambayo inatarajiwa kurindima vilivyo kwenye clubs na sehemu mbalimbali za starehe ndani na hata nje ya Tanzania.

Kilichovutia zaidi ni namna ambavyo midondoko ya sauti ya Abdu na Alikiba imeweza kukaa vizuri sana kwenye beat moja.

Yogo Beats ambaye aghalabu uhusika kuandaa miradi ya kimuziki ya Alikiba ndiye aliyeshughulikia kutengeneza mdundo wa ngoma hii ambayo ni ujio mpya kabisa wa Abdu Kiba baada ya kujichimbia studio kwa takriban miezi saba bila kuachia ngoma ya peke yake.

Kando na ngoma hii, Abdukiba na Alikiba wameshafanya ngoma mbalimbali kwa pamoja ikiwemo ‘Kidela’ pamoja na ngoma ya ‘Single’.

https://www.youtube.com/watch?v=czLdn4oDN1A

Leave your comment