Harmonize Atangaza Kuachia Video Tatu Kutoka Kwa Albamu ya ‘High School’

[Picha: Tuko]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki wa bongo Harmonize ametangaza kuwa anaenda kuachia video tatu kwa pamoja kutoka kwa albamu yake ya ‘High School’.

Harmonize aliachia albamu ya ‘High School’ hivi maajuzi na imepata mapokezi mazuri miongoni mwa mashabiki.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nandy ft. Marioo ‘Kufuli’, Mbosso ft. Zuchu ‘For Your Love’ na Ngoma Zingine Mpya Bongo Wiki Hii

Albamu hiyo ilikuwa na jumla ya ngoma ishirini ila zote zilikuwa katika mfumo wa 'audio'. Baada ya kuachia albamu hiyo ambayo ni ya pili kutoka kwake, Harmonize kwa sasa yumo mbioni katika kutengeneza video ya nyimbo hizo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize aliwaomba mashabiki wake ushauri katika kutoa maoni yao kuhusu nyimbo wanazotaka video zao ziachiwe.

Soma Pia: Hussein Machozi Asifu Albamu ya Harmonize

Msanii huyo, hata hivyo, hakufichua ni ngoma gani tatu kati ya ishirini kwenye albamu yake ambazo zimefanyiwa video.

"(3) Videos one day. Let's go drop me your top 3 from #highschool we go live," chapisho la Harmonize kwenye mtandao wa Instagram lilisomeka.

Harmonize vile vile hakutaja siku wala tarehe kamili ambayo video hizo tatu zitatoka. Mashabiki wake wamesalia na hamu sana huku wakisubiri kuona ni nyimbo gani ambazo zitazawadiwa na video.

Konde Boy, kama anavyofahamika miongoni mwa mashabiki wake, ni mmoja wa wasanii wakubwa kutoka bongo ambao wameachia albamu zao mwaka huu. Albamu yake ilitoka muda mfupi baada ya Alikiba kuachia yake pia.

Albamu ya Alikiba iliyopewa jina la ‘Only One King’ vile vile ilipokelewa vizuri. Wadau mbali mbali wamekuwa wakilinganisha uzito na ubora wa albamu hizo mbili.

Leave your comment