Nyimbo Mpya: Barakah The Prince Aachia Ngoma Mpya ‘Namkumbuka’

[Picha: Ghafla]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki tajika wa Bongo Fleva Barakah The Prince ameachia ngoma mpya inayoitwa ‘Namkumbuka’.

Kama Waswahili wasemavyo kimya kingi huleta mshindo mkuu na bila shaka, Barakah ameendelea kuwaaminisha mashabiki kuhusu ufundi wake kwenye kuandika nyimbo za mapenzi kupitia ngoma hiyo.

Kwenye ‘Namkumbuka’, Barakah anahadithia namna ambavyo anakumbuka mapenzi aliyopewa na mpenzi wake zaman, kwani pamoja na madhila aliyofanyiwa na mpenzi wake huyo, bado anaendelea kutawala na kuchanganya akili yake.

Ngoma hii imepita kwenye mikono ya mtayarishaji na nguli wa muziki kutokea nchini Tanzania wa kuitwa Bob Manecky ambaye ni mtayarishaji wa muziki rasmi wa mwanamuziki Jux, lakini pia ameshafanya kazi na wasanii kama Zee Cuty pamoja na Quick Rocca.

Kwa mwaka huu, hii ni ngoma ya nne kutoka kwa Barakah The Prince. Nyinginezo ni pamoja na ‘Yanatosha’, ‘Rainey’ na ‘Mazima’ zikiwa ni ngoma ambazo zimepokelewa vizuri na mashabiki wa muziki.

Kwa sasa kinachosubiriwa kwa hamu kutoka kwa Barakah The Prince ni Mixtape yake ambayo ameipa jina la ‘Black Prince’ ambayo anatarajia kuiachia muda si mrefu kwa mashabiki zake.

https://www.youtube.com/watch?v=SLZ7LAJF43U

Leave your comment