Mbosso Agoma Kutoa Ngoma Mpya

[Picha: Music in Africa]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea lebo ya WCB Mbosso ameweka wazi kuwa hana mpango wa kutoa ngoma yoyote mpya kwa kipindi cha hivi karibuni.

Mbosso ambaye alitetemesha kiwanda cha muziki Tanzania na albamu yake ya ‘Definition of Love’ mwanzoni mwa mwaka huu, kupitia akaunti yake ya Instagram alichapisha picha ya shabiki aliyebeba bango lililoandikwa "Mbosso tunaomba utoe ngoma mpya tumechoka kusubiri."

Soma Pia: Mkubwa Fella Azungumzia Tetesi za Uhasama Kati ya Mbosso na Aslay

Mbosso alisindikiza picha hiyo na video ya kichekesho kisha akaandika ujumbe uliosomeka "Nasema hivi sitoi wimbo mpya niuweni".

Mara ya mwisho kwa Mbosso kutoa ngoma ilikuwa ni Agosti 7 mwaka huu takriban miezi mitatu nyuma ambapo aliachia ngoma mbili ambazo ni ‘Your Love’ aliyomshirikisha Liya kutokea Nigeria pamoja na ‘Tulizana’ aliyoshirikiana na bendi ya Njenje.

Tangu mwaka huu uanze, Mbosso amekuwa akiachia video ya nyimbo zake kutoka kwenye albamu yake ya ‘Definition of Love’ na kufikia sasa, tayari ameshaachia video nane kutoka kwenye albamu hiyo yenye ngoma 14.

Soma Pia: Diamond Asifia Wimbo wa ‘Inatosha’ Kutoka kwa Lava Lava

Aidha, Mbosso pia amekuwa kwenye orodha ya wasanii kutokea nchini Tanzania ambao wameteuliwa kuwania tuzo za AEAUSA ambapo albamu yake hiyo ya ‘Definition of Love’ imepata nafasi ya kuwania kama albamu bora ya mwaka, sambamba na albamu ya Rayvanny ‘Sounds From Africa’.

Kwenye kipindi hiki ambacho hajatoa wimbo, Mbosso amekuwa akitumbuiza kwenye matamasha mbalimbali ya kimuziki ambapo wiki tatu zilizopita, alikuwa anatumbuiza huko visiwani Zanzibar.

Leave your comment