Diamond Akamilisha Ziara Yake ya Muziki Marekani

[Picha: Sallam SK Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki kutoka Tanzania Diamond Platnumz amekamilisha ziara yake ya muziki nchini Marekani. Meneja wa Diamond Platnumz Sallam SK alidhibitisha kukamilika kwa ziara hiyo kupitia ukurasa wake wa kijamii.

Sallam SK alidokeza kuwa Diamond anajiandaa na huenda ziara yake ifuatayo ikiwa ya bara Ulaya. Ziara ya Diamond Marekani ilianza mnamo tarehe nane mwezi Oktoba katika mkoa wa Atlanta na kukamilika tarehe 31.

Soma Pia: Diamond Asifia Wimbo wa ‘Inatosha’ Kutoka kwa Lava Lava

Diamond alitumbuiza katika jumla ya mikoa kumi na mbili Marekani. Kando na taarifa ya Sallam SK, Diamond bado hajatangaza iwapo kuna kazi ambayo ataendelea nayo Marekani au iwapo atarudi nyumbani Tanzania.

''USA Tour done, thank you everyone! Europe Tour next, be ready!'' Sallam SK aliandika mtandaoni.

Diamond pia anaendelea kutengeneza albamu yake huko Marekani. Utengenezaji wa albamu hiyo umesimamiwa na mtengenezaji wa muziki kutoka Marekani Swizz Beats. Huenda Diamond akabaki Marekani ili kukamilisha albamu hiyo ambayo inatarajiwa kutoka mwaka huu.

Soma Pia: Alikiba, Zuchu, Nandy, Diamond, Harmonize, Rayvanny, Macvoice na Wengineo Wachaguliwa Kuwania Tuzo za AEAUSA

Mpinzani mkuu wa Diamond, Harmonize kwa upande mwingine anaendelea na ziara yake ya muziki huko huko Marekani. Harmonize ndiye aliyekuwa wa kwanza kutua Marekani kwa ziara ambayo ilitarajiwa kudumu kwa muda wa miezi miwili.

Ziara ya Harmonize itakamilika tarehe 26 mwezi huu atakapotumbuiza Dubai. Kwa sasa Harmonize amesalia na sehemu saba za kutumbiza kabal ya kumaliza ziara yake. Harmonize vile vile anatarajiwa kuachia albamu yake tarehe tano mwezi huu.

Leave your comment