20 Percent Amjibu Harmonize Kuhusu Kufanya Collabo

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Twenty Percent hatimaye ameamua kutia neno baada ya Harmonize kuonesha nia ya kufanya nae ngoma ya pamoja siku kadhaa nyuma.

Kwenye mahojiano ya kwanza aliyoyafanya kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, 20 Percent hakutaka kuzungumzia kuhusu taarifa kutoka kwa Harmonize kwani alisema yuko msibani, ila muda mfupi baadae alitumia ukurasa wake wa Instagram upande wa Instastory ambapo aliandika kuwa ‘Ahadi Ni Deni’, akimaanisha kuwa itakuwa ni vyema Harmonize akitimiza ahadi yake hiyo.

Soma Pia: Harmonize Adokeza Kufanya Collabo na Msanii 20 Percent

Ikumbukwe kuwa Harmonize kupitia akaunti yake ya Instagram alionesha nia ya kufanya kazi na mbobezi huyo wa Bongo Fleva, kitu ambacho kilizua furaha na bashasha baina ya mashabiki wa muziki.

Imeshatimia takribani miezi sita sasa tangu 20 Percent atoe ngoma.

Soma Pia: Harmonize Atangaza Tarehe Rasmi Atakayoachia Albamu yake Mpya

Ngoma yake ya mwisho ilikuwa ni ‘Nyumba ya Milele’ aliyomshirikisha EBL Druculla. Hivyo basi, collabo hii na Harmonize inatarajiwa kumtambulisha kwa mashabiki wapya.

Kwa upande wa Harmonize, kwa sasa yuko nchini Marekani kwa ajili ya ziara yake ya kimuziki na hivi karibuni alitangaza kuachia albamu yake ya ‘High School’ tarehe 5 mwezi Novemba mwaka huu.

Leave your comment