Harmonize Adokeza Kufanya Collabo na Msanii 20 Percent

[Picha: Ghafla]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Moja kati ya sifa kubwa aliyonayo Harmonize ni utamaduni wake kushika mkono wasanii wenzake. Hili limethibitishwa zaidi hivi karibuni baada ya kutangaza kuwa atafanya collabo na mwanamuziki 20 Percent.

Harmonize ambaye kwa sasa yuko nchini Marekani ametumia ukurasa wake wa Instagram upande wa Instastory, ambapo alidokeza kuwa mara tu atakapoingia nchini Tanzania, atamtafuta Twenty Percent kwa ajili ya kufanya nae ngoma.

Soma Pia: Harmonize Apendezwa na Album Mpya ya Alikiba 'Only One King'

 "Siku nitakayokanyaga ardhi ya Tanzania hata iwe usiku wa manane Mgoing to the studio with brother 20% Issa dream for me," aliandika msanii huyo.

Harmonize kwa muda mrefu sasa amekuwa na utamaduni wa kufanya ngoma na wasanii wakongwe kutokea nchini Tanzania. Collabo hizo hufanya wasanii hao kufuatiliwa zaidi mashabiki.

 Mathalan, mwaka 2016 Harmonize alifanya ngoma na Dully Sykes ya kuitwa ‘Inde’ kisha miaka miwili baadae wawili hao wakafanya ngoma inayoitwa ‘Kadamshi’ na mwaka 2019, walifanya pamoja ‘Nikomeshe’ ngoma ambayo ilifanya vizuri.

Soma Pia: Ibraah Atangaza Tamasha Jipya ‘Ibraah Homecoming’

Harmonize pia alishafanya ngoma takribani tatu na msanii mkongwe kwenye muziki wa Bongo Fleva Q Chief ambazo ni ‘Go Low’, ‘Nionyeshe’ pamoja na ‘My Boo Remix’.

 20 Percent ni Nani?

Ni mwanamuziki kutokea nchini Tanzania ambaye alikuwa maarufu sana miaka kadhaa nyuma kutokana na kutoa ngoma ambazo zilielimisha sana. Ngoma zake kali ni kama vile; jamii kama vile ‘Ningekusamehe’, ‘Maisha ya Bongo’ na ‘Mama Neema’.

20 Percent anakumbukwa sana baada ya kuweka rekodi ya kubeba tuzo tano kwenye tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards za mwaka 2011 akishinda kama msanii bora wa kiume na mwandishi bora.

Ngoma yake ya ‘Tamaa Mbaya’ ikishinda wimbo bora wa mwaka na ‘Ya Nini Malumbano’ ngoma bora ya Afro Pop kwenye tuzo hizo zilizofanyika jijini Dar es Salaam.

Leave your comment