Harmonize Apendezwa na Album Mpya ya Alikiba 'Only One King'

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bosi wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize amependezwa na kuiunga mkono albamu ya ‘Only One King’ iliyoachiwa na Alikiba.

Mwanamuziki huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliashiria kuwa amependezwa na nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ambayo iliachiwa rasmi hii leo tarehe saba, Octoba.

Soma Pia: Diamond Aondoka Tanzania, Aelekea Marekani kwa Ziara Yake ya Muziki

“Big Tunes,” harmonize alichapisha kwenye Instagram kupitia Insta story.

Ishara ya Harmonize kuipenda albamu ya Alikiba ambaye anakisiwa kuwa mpinzani wake mkuu imewapendeza wengi sana. Harmonize amedhibitisha kuwa kuna upendo na uungaji mkono baina ya wasanii wa bongo licha ya tetesi za uhasama.

Albamu ya Alikiba ambayo iko na jumla ya nyimbo kumi na sita imepokelewa vyema sana na mashabiki. Albamu hiyo imewahusisha wanamuziki kutoka mataifa mbali mbali ya bara la Afrika.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Alikiba Hatimaye Aachia ‘Only One King’ Album

Wakati wa utambulisho wa albamu hiyo, Alikiba alifichua kuwa sababu kuu ya kuitengeneza albamu ilikua kujibu kilio cha mashabiki wake ambao walihisi hafanyi kolabo za kutosha.

Wasanii kutoka Nigeria na Kenya ndio wametawala albamu hiyo, japo pia kuna wengine kutoka mataifa mengine kama vile Ghana.

Harmonize kwa upande mwingine anaendelea na ziara yake ya muziki nchini Marekani. Msanii huyo pia anaendelea kuitengeneza albamu yake ambayo imepewa jina la Arizona The Album.

Tembo, kama anavyojulikana kiusanii, bado hajatoa habari zaidi haswaa kuhusiana na idadi ya nyimbo kwenye albamu hiyo. Albamu yake hata hivyo imesubiriwa kwa hamu ikizingatiwa kuwa Alikiba tayari ashadondosha yake na Diamond Platnumz pia anajiandaa kuachia yake.

Leave your comment