Harmonize Atangaza Tarehe Rasmi Atakayoachia Albamu yake Mpya

[Picha: Ubetoo]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota kutoka bongo Harmonize hatimaye ametangaza tarehe rasmi ambayo ataachia albamu yake iliyosubiriwa kwa hamu sana.

Hapo awali Harmonize alikuwa ameashiria kuwa atadondosha albamu hiyo mwezi huu ila amebadilisha tarehe kwa sababu zisizoepukika.

Soma Pia: Harmonize Adokeza Kufanya Collabo na Msanii 20 Percent

Kwa mujibu wa taarifa ya Harmonize, albamu hiyo iliyopewa jina la 'High School' itatoka mnamo tarehe tano mwezi wa kumi na moja.

Albamu hiyo imesubiriwa kwa hamu sana na mashabiki wa Harmonize. Aidha, bosi huyo wa Konde Music Worldwide hakufichua habari zaidi kuhusu albamu hiyo haswaa kuhusiana na idadi ya nyimbo zilizomo na kolabo alizofanya.

Harmonize kwa upande mwingine amesema kuwa angependa sana kushirikiana na mwanamuziki nyota 20%.

"Siku nitakayo kanyaga ardhi ya Tanzania hata iwe usiku wa manane nitaenda studio na kaka yangu 20%. Hii ni ndoto yangu," Harmonize aliandika mtandaoni.

'High School' itakuwa albamu ya pilii kutoka kwa Harmonize baada ya albamu yake ya kwanza iliyopewa jina la 'Afro East'. Albamu ya 'Afro East' iliyoachiwa mapema mwaka jana ilipokelewa vizuri na mashabiki na kuvuma sana kwenye anga za burudani.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Lava Lava ‘Inatosha’, Nandy ‘Kunjani’ na Ngoma Zingine Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii

Harmonize alikuwa miongoni mwa wasanii wakubwa nchini Tanzania ambao walitangaza kuachia albamu zao mwaka huu.

Tayari Alikiba ashatoa albamu yake ambayo ilipewa jina la 'Only One King'. Diamond Platnumz kwa upande mwingine bado anashughulikia albamu na ziara yake Marekani, hajatangaza tarehe ambayo ataachia albamu yake.

Leave your comment