T.I.D Ajibu Madai ya Kuwepo kwa Ugomvi Baina Yake na Chidi Benz

[Picha: Music in Africa]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki maarufu kutoka nchini Tanzania T.I.D amekana madai ya ugomvi baina yake na msanii Chidi Benz.

Licha ya wasanii hawa wawili kuwa na ukaribu mno, tuhuma za ugomvi baina yao zimewaandama kwa muda sasa. Wawili hao pia kwa sasa wako na kipindi ambacho wanaendesha pamoja na kinapeperushwa kwenye runinga.

Soma Pia: Chid Benz Asifu Rapa wa Kenya Khaligraph Jones kwa Kipaji Chake

Wadau mbali mbali wamedai kuwa huenda tofauti baina yao ikaathiri kipindi hicho. T.I.D akizungumza wakati wa mahojiano na Wasafi FM alisema kuwa hakujawahi kuwa na ugomvi kati yake na Chidi Benz.

 Alifafanua kuwa Chidi Benz ni mtu ambaye anapenda kuzungumza kwa sauti sana na kusikika ila amejifunza kuishi na yeye.

Kwa mujibu wa T.I.D, tuhuma hizo zinatokana na tetesi zisizokuwa za kweli ambazo ziliibuka kwenye mitandao.

Soma Pia: Chidi Benz Adai Kuna Uhasama Baina ya Tunda Man na Diamond Platnumz

"Mimi hata sijui kama nimewahi kupishana kauli na Chidi Benz. Sijawahi kwanza, wewe hizo habari umepata wapi... Acheni mambo ya kutunga tunga. Mimi na Chidi Benz matatizo yoyote. Ingawa tu saa ingine anakuanga loud voice, but if you learn to live with somebody, you know this is how you are suppossed to live, munaishi hivyo. Usikorofishane na mtu tu kwa sababu watu wanasema yeye ndiye mkorofi ata kama hajakukorofisha," T.I.D alisema.

T.I.D aliongezea kuwa anafanya kazi vyema na Chidi Benz kupitia mkataba wa mwaka mmoja walioupata wa kufanya kipindi cha Maskani Poa.

Leave your comment