Diamond Apata Mafanikio Makubwa Kwenye Tamasha Lake Marekani

[Picha: All Africa]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania Diamond Platnumz anazidi kupata mafanikio makubwa nchini Marekani kupitia ziara yake ya muziki.

Tukio moja ambalo limedhihirisha mafanikio yake kwenye ziara hiyo ni yeye kuuza tiketi zote za onyesho lake. Hili ni jambo ambalo limewagusa wadau wengi kwenye tasnia ya muziki ambao wamemmiminia sifa Diamond Platnumz.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Diamond Platnumz Aachia ‘Gimme Dat’ Akimshirikisha Rema

Diamond kuuza tiketi zote za onyesha hilo kumeandikisha historia katika taaluma yake ya muziki na pia kuonyesha kuwa ako na ufuasi mkubwa katika taifa la Marekani.

Tayari Diamond ameshatumbuiza katika mikoa miwili ambayo ni Atlanta na Washington. Msanii huyo pia alizidia kuwasihi mashabiki wake kujitokeza na kumuunga mkono katika maonyesho yake yatakayo fanyika katika mikoa mingine.

Kwa mujibu wa ratiba ya ziara ya Diamond, amesalia na jumla ya maonyesho kumi na moja ambako atajumuika na kutumbuiza mashabiki wake.

Soma Pia: Sababu Tano Kuu Zinazoeleza Mbona Tasnia ya Muziki ya Tanzania Inahitaji Tuzo Za Kinyumbani

"Update your city calendar! Minneapolis , Minnesota Oct 15th Friday Denver Oct 16th Saturday Los Angeles Sunday!" chapisho la Diamond mtandaoni lilisomeka.

Wakati Diamond anazidi kuandikisha mafanikio kwenye ziara yake, mwenzake Harmonize ambaye pia yuko kwenye ziara ya muziki Marekani vile vile hajaachwa nyuma.

Maonyesho ya Harmonize pia yamehudhuriwa na idadi nzuri ya mashabiki. Mafanikio ya wasanii hawa wawili yameashiria kuwa muziki wa kiafrika umepenya katika taifa la Marekani na umeanza kukita mizizi miongoni mwa watu huko.

Leave your comment