Nyimbo Mpya: Diamond Platnumz Aachia ‘Gimmie’ Akimshirikisha Rema

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Diamond ameachia ngoma mpya yenye jina ‘Gimmie’ akimshirikisha nyota kutokea Mavin Records ya nchini Nigeria Rema.

Diamond Platnumz anafungua ngoma hii akimsifia mrembo wake namna ambavyo anampa mapenzi moto moto. Diamond anatumia sauti yake ya kuvutia kumuelekeza mpenzi wake jinsi ya kucheza kwa usahihi ili azidi kumpagawisha zaidi.

Soma Pia: Sababu Tano Kuu Zinazoeleza Mbona Tasnia ya Muziki ya Tanzania Inahitaji Tuzo Za Kinyumbani

Rema anapokea kijiti kwenye aya ya pili ya ngoma hii akizidi kutoa sifa kwa mpenzi wake.

"Say me i wanna tell you my story many many drama many many girls me wanna come in ma way, I say they would come for the money, girl I wanna flex" anaimba Rema kwenye aya ya pili.

Tofauti kabisa na ‘Naanzaje’, wimbo wa ‘Gimmie’ una vionjo vya Afro Beats na ni wimbo ambao unatarajiwa kufanya vizuri sana kwemye clubs na sehemu mbalimbali za kustarehe barani Afrika.

Soma Pia: Diamond Platnumz Atuzwa Msanii Bora wa Afrika

Lizer Classic kutokea Wasafi Records ndiye amehusika kufanya maandalizi ya mwisho ya ngoma hii.

Tetesi za uwepo wa ngoma baina ya Diamond Platnumz na Rema zilianza kushika kasi Oktoba mwaka 2020 baada ya msanii Rema kuja Tanzania.

Akiwa kwenye show yake aliyofanya ukumbi wa Elements Dar es salaam, Rema aligusia kuhusu kufanya ngoma na Diamond Platnumz kisha siku chache baadae wawili hao kupitia mitandao ya kijamii walionekana wakiwa wanafanya video ya ngoma hiyo.

Huu ni muendelezo wa Diamond Platnumz kuwa na utamaduni wa kupendelea kufanya ngoma na wasanii kutokea Nigeria. Kufikia sasa, Simba ameshafanya kazi na wasanii wengi wa Nigeria kama Davido, Iyanya, Teni, Mr Flavour, Patoranking na wengineo wengi.

https://www.youtube.com/watch?v=nKSVX3mdfiA

Leave your comment