Madee Seneda Afunguka Sababu ya Kuachia Wimbo Mmoja kwa Mwaka

[Picha: Popnable]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa kutokea nchini Tanzania Madee Seneda hivi karibuni ameeleza sababu za kuwa na utamaduni wa kutoa wimbo mmoja tu kwa mwaka.

Madee ambaye ni mojawapo ya wasanii wa Hip-hop wakongwe hapa nchini Tanzania amekuwa na utaratibu wa kuachia ngoma moja tu kwa mwaka na mathalani mwaka huu bado rapa huyo hajaachia ngoma yoyote.

Soma Pia: Collabo Tano Kali Alizofanya Patoranking na Wasanii wa Bongo

Wimbo wake wa mwisho ulikuwa ni ‘Hadithi 2060’ alioachia mwezi Agosti mwaka 2020.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL, Madee ametanabaisha kuwa hapendelei kutoa nyimbo mara kwa mara kwa sababu anataka awape nafasi wasanii wachanga nao wapate fursa na na nafasi ya kuonekana zaidi.

Soma Pia: Mac Voice Aeleza Wosia Aliopewa na Diamond Kipindi Alijiunga na Next Level Music

"Mimi kwa mwaka huwa natoa kibao kimoja tu. Sinaga kuhangaika hangaika sana kama vile nimeanza muziki leo. Inabidi tuweke gap ambayo itafaa waonekane na watu wengine. Mi tayari sina cha kupoteza mpaka sahizi mshanisikia sana watu wananielewa tukiwapa nafasi underground basi tunakuwa tunaupa nafasi pia muziki wetu wa Bongo Fleva uwepo kwa muda mrefu," Madee alinena.

Mwanamuziki huyo aliongeza kwa kusema kuwa wakati ambao hafanyi muziki, yeye hujishughulisha sana na biashara za kununua magari kutoka nchi kama Japan na kuyauza hapa Tanzania.

"Nafanya biashara biashara zangu. Especially biashara za magari. Namaanisha kwamba naagiza magari then nauza magari. Ninayo show room kubwa tu naagiza Japan. Nadhani ni kitu ambacho nakipenda toka zamani," alizungumza Madee.

Ukiweka kando ngoma zake kama ‘Paulina’, ‘Pombe’ na ‘Sema’ zilizoteka hisia za wapenda muziki hapa nchini Tanzania, Madee pia husifika kwa uwezo mkubwa wa kukuza na kulea vipaji vya wasanii kama Dogo Janja pamoja na Rayvanny ambao kwa sasa ni wasanii wakubwa sana hapa Tanzania.

Leave your comment