Harmonize Amsifia Cheed kwa Uwezo na Uhalisia Wake Ndani ya 'Wandia'

[Picha: Cheed Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bosi wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize ameelezea kupendezwa na talanta ya msanii Cheed ambaye amesainiwa chini ya lebo yake.

Harmonize kupitia ukurasa wake wa Instagram alimsifu Cheed kama mwanamuziki mwenye uhalisia na uwezo mkubwa ikija kwa muziki. Tembo, kama anavyojulikana kiusanii, alikiri kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa msanii Cheed.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Alikiba ‘Oya Oya’, Mac Voice ‘Tamu’ na Ngoma Zingine Zinazotamba Bongo Wiki Hii

Aliendelea kwa kusema kuwa anaaminia uwezo wa Cheed na angependa dunia nzima imfahamu.

Msanii huyo aliupigia wimbo mpya wa Cheed kampeni na kuwahimiza wafuasi wake wakautazame. Kwa mujibu wa Harmonize, wimbo wa Cheed wa 'Wandia' ni ngoma yenye hadithi tamu ya mapenzi.

"I'm big fan of you my brother @officialcheed natamani dunia ijue…Na kupitia hii ngoma nimejikuta natambua uwezo wako mwingine wa kuvaa uhalisia. My people who is watching this with me now?" chapisho la Harmonize mtandaoni lilisomeka.

Soma Pia: Sababu Nne Kuu Zinazowafanya Wasanii Wengi Tanzania Kuanzisha Lebo za Muziki

Cheed ndio msanii mpya kabisa kutoka Konde Music Worldwide na alidondosha ngoma yake ya kwanza kwa jina la 'Wandia' siku chache zilizopita. Maswali hata hivyo yameibuka kuhusu kucheleweshwa kwa Cheed.

Licha ya kutambulishwa mwaka jana kama mwanachama wa Konde Music Worldwide, Cheed alisubiri kwa takriban mwaka mmoja kabla ya kutoa kazi yake ya kwanza.

Cheed hapo awali alikuwa amesainiwa chini ya lebo ya Kings Music inayomilikiwa na Alikiba kabla ya kuhamia Konde Music Worldwide.

Leave your comment