Mac Voice Ajibu Madai ya Ugomvi Baina ya Chege na Rayvanny

[Picha: Rayvanny Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii chipukizi Mac Voice hatimaye amefunguka kuhusu uhusiano uliopo baina ya Rayvanny na Chege baada ya tetesi kuashiria kuwa huenda wawili hao wako na ugomvi.

Kwa mujibu wa tetesi hizo, Mac Voice ndiye chanzo cha ugomvi kwani kabla ya kuenda katika lebo ya Next Level Music inayomilikiwa na Rayvanny, alikuwa chini ya usimamizi wa Chege.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Mac Voice, Cheed, Barnaba na Wasanii Wengine Bongo Wiki Hii

Akizungumza wakati wa mahojiano katika kipindi cha Big Sunday Live, Mac Voice alikanusha madai hayo na kusisitiza kuwa hakuna ugmovi kati ya Rayvanny na Chege.

Alieleza kuwa Chege na Rayvanny wako na ukaribu mno na hivyo basi hawawezi kukosana kwa sababu yake. Alikiri kuwa, alikuwa akifanya kazi na Chege ila yeye kuhamia Next Level haikuleta tofauti zozote.

"Chege ni brother yangu na atabaki kuwa brother yangu milele na atabaki kukuwa familia yangu milele. Lakini kukusahihisha katika suala lako, Chege, Madee na Rayvanny ni familia moja, kwa hiyo hakuna tatizo na ndio maana kama ukipita kwa post ya chege ameniposti," Mac Voice alisema.

Mac Voice amekua mada kuu miongoni mwa wadau mbali mbali katika tasnia ya burudani nchini Tanzania tangu kutambulishwa kwake kama msanii wa kwanza chini ya Next Level music.

Soma Pia: Diamond, Rayvanny, Harmonize, Zuchu na Mbosso Waongoza Wasanii Waliotazamwa Zaidi YouTube Tanzania Mwezi Septemba

Aidha, msanii huyo ametoa EP yake ya kwanza yenye nyimbo sita na imepokelewa vizuri sana na mashabiki.

Lebo ya Next Level Music inaendela na harakati ya kumtambulisha Mac Voice, na kwa sasa anafanya 'media tour'.

Leave your comment