Babu Tale Amtetea Harmonize Baada ya Tamasha Yake Marekani Kuhudhuriwa na Watu Wachache

[Picha: Ghafla]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Meneja wa Diamond Platnumz Babu Tale amemtetea Harmonize kwa kile kilichoonekana kama show za kwanza za msanii huyo huko nchini Marekani kutopata wahudhuriaji wengi.

Harmonize kwa sasa yuko nchini Marekani kwa ajili ya ziara yake ya kimuziki na kipindi anaanza ziara yake nchini humo, kuna baadhi ya video zilikuwa zikisambaa mtandaoni zikionesha mwitikio mdogo wa watu kwenye tamasha la msanii huyo.

Soma Pia: Meneja wa Harmonize Azungumzia Mapokezi Waliyopata Katika Ziara Yao Marekani

Akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni, Babu Tale amewakosoa vikali wanaomkosoa Harmonize kwa show yake hiyo kukosa watazamaji wengi.

"Harmonize kama Harmonize anapambana na anapambana kukuza lugha ya Kiswahili kwa hiyo anaembeza hajui anachopitia Harmonize kwenye kupambana kukuza lugha ya Kiswahili," alizungumza Babu Tale.

Babu Tale pia aliongeza kuwa Harmonize asilalamikiwe na asishindanishwe na wasanii wanaotumia lugha ya Kiingereza kwani Marekani watu wengi huzungumza kiingereza.

Soma Pia: Babu Tale Azungumzia Diamond Kulinganishwa na Wasanii wa Nigeria

"Mtu ametoka kwenye Swahili nation anakwenda kupambana kukuza kiswahili wamekuja watu wachache kwenye event yake wewe unamlalamikia? Unakwenda kumcompete na wasanii wanaoongea kizungu ni huzuni tu," aliongea Babu Tale.

Aidha kwenye mahojiano hayo, Babu Tale alihakikishia wanahabari kuwa msanii wake Diamond Platnumz ana kazi nyingi ambazo ziko kapuni na ni suala la muda tu zitaingia sokoni.

Leave your comment