Meneja wa Harmonize Azungumzia Mapokezi Waliyopata Katika Ziara Yao Marekani

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Meneja wa Harmonize ambaye anafahamika kama Mjerumani amefunguka kuhusu mapokezi ambayo Harmonize na timu yake walipata marekani katika ziara yake ya Muziki.

Soma Pia: Harmonize Ampongeza Killy Baada ya Ngoma Yake 'Ni Wewe' Kupata Mafanikio Makubwa

Mjerumani ni mmoja wa wasimamizi wa Harmonize ambao wako kwenye ziara hiyo.

Hivi karibuni, tetesi ziliibuka mtandaoni kwamba huenda Harmonize hakupata mapokezi mazuri kama alivyotarajia. Mjerumani hata hivyo amekanusha madai hayo na kusisitiza kuwa Harmonize amepata mafanikio mazuri Marekani.

Mjerumani alifichua kuwa ziara ya Harmonize imeandaliwa na mapromota wa Marekani na hivyo basi wamehakikisha kuwa mashabiki wanahudhuria tamasha hizo.

Kwa mujibu wa Mjerumani, wako na timu ya mapromota katika majimbo tofauti ambako Harmonize anatarajiwa kutumbuiza.

Soma Pia: Meneja wa Harmonize Ajibu Wakosoaji Wanaomsema Msanii Huyo Vibaya 

"Kwanza niwakumbushe tu kwamba hizi show ambazo Harmonize anazifanya, hii tour, ni tour ambayo imeandaliwa na ma promoters kutoka majimbo tofauti ya Marekani. Kwa hivyo ni show ambazo zimenunuliwa, yaani Harmonize analipwa, kwa hiyo promotions na targets zimewekwa na promoter kulingana na taarget ambayo anataka kuifikia," Harmonize alisema.

"So far tangia tumefika tumeshafanya show tatu na mapokezi yalikuwa mazuri sana. Kwa sababu tumepata pia mashabiki wetu kutoka nchi tofauti ambao wako huku na wameshiriki show. Kwa hiyo kwetu sisi tumechukulia ni sign kwamba muziki wetu unasikilizwa pia na mataifa mengine, umefika mbali na kitu ambacho kimetu impress sana na tunaona kwamba soko letu sasa hivi lime penetrate so tuko vizuri sana kwa maana ya industry," Mjerumani aliongezea.

Leave your comment