Harmonize Ampongeza Killy Baada ya Ngoma Yake 'Ni Wewe' Kupata Mafanikio Makubwa

[Picha: Bongo 5]

Mwandishi: Brian SIkulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki wa bongo Harmonize amempongeza msanii chipukizi Killy kwa mafanikio ambayo wimbo wake wa 'Ni Wewe' umepata. Killy aliachia ngoma ya 'Ni Wewe' akimshirikisha Harmonize takriban wiki mbili zilizopita na kufikia sasa ishatazamwa mara milioni moja kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Cheed Atangaza Tarehe Atakayoachia Ngoma Yake Ya Kwanza Chini Ya Konde Music Worldwide

Ngoma hiyo iliachiwa kwa mtindo wa audio bila video na kwa hivyo kupata idadi kubwa ya watazamaji kunaashiria kuwa video yake pia itapata mafaniko makubwa ikitoka.

Aidha, Harmonize wakati anampongeza Killy kupitia chapisho kwenye ukurasa wake wa Instagram, aliashiria ujio wa video ya wimbo huo

Harmonize vile vile alichukua fursa hiyo kuwakumbusha mashabiki wake kuhusu kazi mpya inayotarajiwa kutoka kwa msanii Cheed hapo kesho. Cheed atakua anaachia kazi yake ya kwanza chini ya lebo ya Konde Music Worldwide tangu yeye kutambulishwa mwaka jana.

Soma Pia: Anjella Afunguka Kushindanishwa na Zuchu, Nandy

Hapo awali Cheed na Killy walikua wanachama wa lebo ya Kings Music kabla ya kuhamia Konde Music Worldwide.

"Congrats fundiiiii @officialkilly_tz  for one million ukizingatia ni audio peke ...!!! Who is ready for da movie ? Killy ft tembo #niwewe. Najua ni kwakiasi gani umekuwa ukisubiri mawe ya kijana mwenzio yaanze kutoka and finally we here let's go my people Cheed day almost here," Harmonize aliandika mtandaoni.

Leave your comment