Country Wizzy Afunguka Konde Gang Ilivyobadilisha Maisha Yake Kimuziki

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa kutokea Tanzania Country Wizzy amefunguka jinsi maisha yake ya kimuziki yamebadilika tangu alipoingia kwenye lebo ya Konde Music Worldwide. Country Wizzy alitambulishwa kama msanii rasmi wa Konde Gang Septemba mwaka jana.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni, rapa huyo amefunguka kuwa kuwepo chini ya lebo hiyo imemuongezea thamani kama msanii, na hata wasifu pia kama msanii wa rap umepanda kwa kiasi kikubwa.

Soma Pia: Maua Sama Azungumzia Collabo yake na T Pain, Aeleza Sababu Hajaachia Kazi Hio Bado

"Kufanya kazi na Konde Gang imeongeza impact na thamani kwa sababu unakuwa ni msanii ambaye uko under record label tayari kuna vitu vinapungua like majukumu mengine mi nakuwa siyafanyi inafanya management kwa hiyo nakuwa msanii ambaye niko protected sana," alizungumza msanii huyo.

Aidha, Country Wizzy aliongeza kuwa yeye kuwepo Konde Gang hata hadhi ya muziki wa rap umepanda kwani mara nyingi wasanii wa Hip-hop huwa wanakosa nafasi ya kujiunga na lebo kubwa.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Diamond, Rosa Ree, Beka Flavour na Wasanii Wengine Bongo Wiki Hii

“Imeongeza thamani pia ya rap music sio tu mimi hadi muziki wa rap na nategemea tu kuna wasanii wengi pia watapata deals kwenye record labels mbalimbali na pengine record labels nyingine pia zitafungua kwa ajili ya kumanage wasanii wa rap," alizungumza Country Wizzy.

Kwenye lebo ya Konde Gang, Country Wizzy ndiye msanii pekee anayefanya muziki aina ya Hip-hop. Kabla kuingia kwenye lebo hiyo, Wizzy alipita kwenye lebo kadhaa ikiwemo Rooftop Entertainment.

Kwenye mahojiano hayo pia, Country kwa upande wake alimtaja Mangwair kama msanii bora wa Hip-hop nchini Tanzania.

Leave your comment