Rayvanny ‘Wanaweweseka’, Jux ‘Sina Neno’ na Nyimbo Zingine Zinazotamba Bongo

[Picha:YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wiki nyingine tena ya mwezi Septemba na kwenye kiwanda cha muziki hapa Tanzania, mambo yameendelea kuwa sukari hasa kwenye mtandao wa YouTube ambapo wasanii wengi huweka kazi zao. Zifuatazo ni nyimbo tano ambazo zimepata mwitikio mzuri zaidi YouTube Tanzania wiki hii:

Soma Pia: Diamond Platnumz, Zuchu, Nandy Alikiba, Darassa, Harmonize na Rayvanny Watajwa Kuwania Tuzo Za AFRIMA 2021

Naanzaje - Diamond Platnumz

Mwanamuziki Diamond Platnumz kwa wiki ya pili mfululizo ameendelea kushika namba moja kwenye mtandao wa YouTube na ngoma yake ya ‘Naanzaje’ . Kwenye wimbohuu, Diamond anamhaidi mpenzi wake kuwa watakuwa pamoja milele bila kuachana. Mpaka sasa video ya ngoma hii imeshatazamwa mara milioni 6.7 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=iKbW2EDs_mE

Wanaweweseka – Rayvanny

Barua ya mapenzi ya Rayvanny kwa mpenzi wake kupitia ngoma ya ‘Wanaweweseka’ inaendelea kufanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube. Kufikia sasa, kazi hii iliyotayarishwa na Lizer Classic kutokea Wasafi Records imeshatazamwa mara milioni 2.8 kwenye YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=M6WisT8ocUE

Sina Neno - Jux

Ilipofika tarehe 22 ya mwezi huu, Jux alipoza kiu ya mashabiki zake baada ya kuachia video ya ‘Sina Neno’ ambayo ilisubiriwa kwa hamu sana na wapenda muziki. Director Hanscana ameweza kufanya kazi nzuri sana katika kuaandaa video hii ambayo ndani ya siku mbili tu imeweza kuzoa watazamaji laki nne tisini kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=cDxZrTIcKLk

Beer Tamu - Marioo

Marioo hajawahi kukosea pale anapokutana na mdundo wa Amapiano na ngoma yake ya hivi karibuni ‘Beer Tamu’ imeendelea kuthibitisha hilo. Ngoma hii inafanya vizuri sana kwenye baa, clubs na sehemu za starehe na hata kwenye mtandao wa YouTube pia.

https://www.youtube.com/watch?v=ACjpKIU973Y

Teacher - Harmonize

Wiki tatu baada ya kuachia video ya ‘Teacher’, Harmonize ameendelea kuthibitisha kuwa yeye ni Mwalimu na mkufunzi aliyebobea kwenye muziki wa Amapiano kwani ngoma hiyo bado inafanya vizuri mtandaoni. Kufikia sasa, ‘Teacher’ imeshajizolea watazamaji takribani milioni 4.4 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=mPVoKSc6LJo

Leave your comment