Nyimbo Mpya: Rich Mavoko Aachia Video ya ‘Ndo Maana’

[Picha: Nairobi News]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki maarufu kutokea Tanzania Rich Mavoko hatimaye ameachia video ya wimbo wake ‘Ndo Maana’.

Rich Mavoko ambaye hupendelea kuitwa Bilionea Kid, ameachia video hiyo ikiwa imeshapita takriban wiki nne tangu aachie audio ya wimbo huo, ambayo imetayarishwa na nguli wa muziki Tanzania Aby Dady.

Soma Pia: Rich Mavoko Awashauri Wasanii Dhidi ya Kununua Watazamaji YouTube

Video ya ‘Ndo Maana; imejaa ubunifu, uhalisia pamoja na stori nzuri ambapo Rich Mavoko anaonekana akiwa na marafiki zake wakienda sehemu kula raha, lakini kutokana na kuumizwa na mapenzi, Mavoko anakosa raha kwani kila mara anamkumbuka mpenzi wake wa zamani.

Kwenye audio ya wimbo huu, Rich Mavoko alionekana kusimulia maumivu anayopitia, lakini ndani ya video hii, wahusika wamejawa na nuru, uchangamfu pamoja na raha. Bila shaka, video hii ni mojawapo kati ya kazi bora kutoka kwa Rich Mavoko.

Soma Pia: Rich Mavoko Azungumzia Tofauti Baina yake na Diamond Platnumz

Kampuni iliyohusika kuandaa video hii ni Edible Elevens ambayo pia ni kampuni iliyoshiriki kuandaa video ya Alikiba ‘infedele’, ‘Nakupenda’ ya DJ Sbu pamoja na Alikiba pamoja na ‘Proud of You’ ya Darassa ft Alikiba.

Kwa mwaka huu, ‘Ndo Maana’ ni video ya tatu kutoka kwa Rich Mavoko kwani mwezi Mei aliachia video ya ngoma yake ‘Mapenzi’ na mwezi Julai aliachia ‘Nidonoe’ ngoma ambayo pia ilifanya vizuri sana sokoni.

https://www.youtube.com/watch?v=QzPg2gslxuA

Leave your comment