Chege Aeleza Sababu Ya Kuepuka Kufanya Muziki Wa Amapiano

[Picha: Chege Instagram ]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii kutokea nchini Tanzania Chege ameeleza kwa kina sababu ya yeye kutokufanya muziki wa Amapiano ambao unatamba sana hapa Tanzania kwa sasa kutokana na wasanii kupenda kufanya aina hiyo ya muziki. Kwenye mahojiano aliyoyafanya na kituo cha Wasafi TV hivi karibuni Chege ameeleza kuwa hajataka tu kufanya aina hiyo ya muziki kwani alishafanya muziki wenye asili ya Afrika kusini miaka kadhaa nyuma.

Soma pia: Diamond Platnumz, Zuchu, Lavalava, Mbosso Wamkaribisha Msanii Mpya Wa Rayvanny Mac Voice

"Nimejisikia tu nisiufanye kiukweli kabisa. Ndoaana natoa ngoma za aina nyingine kabisa. Mi nishafanya miziki ya kisouth Africa longtime. Nimefanya sana. Kwa hiyo mi nimeamua tu kuachana nazo" alizungumza Chege. 

Ikumbukwe kuwa Chege miaka kama mitano nyuma alikuwa anatoa kwa wingi ngoma ambazo zina mahadhi ya Afrika Kusini kama vile "Kaunyaka" ft Mh Temba & Maphorisa, "Sweety Sweety" ft Runtown & Uhuru pamoja na "Waka" aliomshirikisha Xelimpilo. Kwenye mahojiano hayo Chege alizidi kudokeza kuwa alikuwa anatumia muda mwingi sana nchini Afrika kusini kutengeneza ngoma na kufanya video ikafikia kipindi watu wakamwambia asitishe kwanza utoaji wake wa ngoma.

. "Mi nilikuwa nakaa huko huko (South Africa) miezi mitatu minne nakaa tu nafnya mamgoma nashoot mavideo narudi natoa hadi baadae kuna watu walijitokeza wakawa wanasema bwana hatutaki ngoma za Kisouth Africa. Nikaja kushangaa tena sahivi ndo zimekuja kuwa ndo ngoma noma"alizungumza Chege.

Kwa sasa Chege anatamba na ngoma yake ya "Kushki" aliyomshirikisha mwanadada Saraphina.

https://www.youtube.com/watch?v=TttpK5SjXb8

 

 

 

Leave your comment