Young Lunya Aweka Wazi Tetesi Kuhusu Collabo Yake na Diamond Platnumz

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa kutokea nchini Tanzania Young Lunya amefunguka kuhusu tetesi ya kuwa ameshafanya ngoma ya pamoja na bosi wa Wasafi Diamond Platnumz.

Soma Pia: Rayvanny Amtambulisha Msanii wa Kwanza wa Next Level Music

Akiongea kwenye mahojiano aliyofanya na Lil Ommy hivi karibuni, Lunya alisema kuwa wawili hao bado hawajaingia studio kurekodi ngoma ya pamoja ila kulikuwa na mpango wa kuwepo kwa collabo baina ya pande zote mbili.

"Diamond tumeplan kufanya kazi muda mrefu sana lakini nafikiri tu yuko busy na nini lakini ni kitu ambacho kipo kabisa yani tulishaplan lazima tufanya madude moja ya kwake mojavya kwangu Niko kwenye process nasubiria tu adondoke kutoka marekani tuue," aliongea Young Lunya

Hoja ya Young Lunya kufanya ngoma na Diamond Platnumz ilipamba moto kuanzia mwezi Aprili mwaka huu baada ya msanii huyo kuchapisha picha kwenye akaunti yake ya Instagram akiwa pamoja na Diamond Platnumz na S2kizzy na kuandika "Bet y'all want Diamond in my album. Niko nae hapa anything can happen," aliandika Lunya.

Soma Pia: Nandy Azungumzia Changamoto za Kuandaa Matamasha

Kwa muda mrefu sasa, Young Lunya amekuwa akidokeza kuhusu ujio wa albamu yake ambayo kufikia sasa ameshathibitisha kuwa rapa Joh Makini toka kundi la Weusi atashirikishwa kwenye albamu hiyo.

Kwa sasa, Lunya anatamba kwenye ngoma aliyoshirikishwa na Maua Sama ‘Away’ ngoma ambayo imependwa sana na wapenzi mbalimbali wa muziki Tanzania kutokana na mashairi yake kuwa mazuri.

Leave your comment