Meneja wa Harmonize Ajibu Wakosoaji Wanaomsema Msanii Huyo Vibaya

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Meneja wa Harmonize ambaye anafahamika kama Chopa hatimaye amefunguka kuhusu msanii wake kukumbwa na ukosoaji mwingi mtandaoni kwa siku za hivi karibuni. Baadhi ya tetesi zilizoko miongoni mwa wakosoaji wa Harmonize ni kuwa huenda ziara yake ya muziki huko Marekani haijapata mafanikio kama ilivyotarajiwa hapo awali.

Japo tetesi hizo zimesambaa mitandaoni, chapisho za Harmonize zimedhibitisha kuwa ziara yake inaendelea bila matatizo yoyote na amepokelewa vizuri na mashabiki wake katika mikoa tofauti Marekani.

Soma Pia: Harmonize Atangaza Ujio wa Albamu Mpya ‘Arizona’

Chopa akizungumza na wanahabari, alisema kuwa si jambo geni msanii mkubwa kama Harmonize kukashifiwa mitandaoni. Aliongeza kuwa wapo wanaomkashifu Harmonize ili wapate umaarufu.

"Usipomzungumzia vibaya Harmonize utamzungumzia nani. Kwa sasa ilipofikia, ili uzungumziwe na wewe lazima umzungumzie vibaya Harmonize, kwa hivyo vitu negative sio Harmonize tu anakutana navyo. Karibia kila mtu anakutana navyo lakini inapishana na ukubwa.

“Na sisi izi comment negative tunaziitaji kwa wingi zaidi, kwa sababu mtu anavyozungumziwa vibaya ndio unajuwa kabisa kwamba ana impact. Mtu ambaye hana impact huwezi ukamzungumzia. Kwa hiyo ili utrend sasa hivi unastahili umzungumzie Harmonize, usipomzungumzia sasa hivi huwezi kufanya vizuri," Chopa alisema.

Soma Pia: Meja Kunta Atangaza Ujio wa EP Yake Mpya

Harmonize yupo nchini Marekani ambako anaendelea na ziara yake ya muziki. Kufikia sasa ametumbuiza katika mikoa kadhaa na mapokezi yake yameonekana kuwa mazuri. Ziara hiyo inatarajiwa kudumu kwa muda wa miezi miwili.

Leave your comment