Maua Sama na Young Lunya Wadokeza Ujio wa Ngoma Mpya

[Picha: Maua Sama Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Dalili zote zinaonesha kuwa malkia wa RnB nchini Tanzania Maua Sama anarudi tena kwa kishindo kwenye soko la muziki baada ya kudokeza  ujio wa ngoma yake mpya ambayo ameshirikiana na rapa Young Lunya kutokea Intersource Records.

Soma Pia: Maua Sama Afunguka Kuhusu Tatizo la Kiafya Lilioathiri Utendakazi Wake Kimuziki

Mapema leo, Maua Sama pamoja na Young Lunya wote wamechapisha kwenye akaunti zao za Instagram ikiwaonesha wakiwa wanavuka barabara huku wakiwa wamejifunika na mablanketi yenye rangi nyeupe.

Maua Sama amesindikiza picha hizo kwa kuandika ‘Na itatokea kesho 8:30 Am’ kisha akamtag Young Lunya ambaye nae aliandika ujumbe unaofanana na huo.

Taarifa hii inakuja siku chache baada ya Maua Sama kutangaza kuwa anarudi kwenye muziki baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu sasa kutokana na kuwa na kupatwa na tatizo la kiafya la kutosikia vizuri na matatizo mengine yalioathiri kinywa chake.

Soa Pia: Wasifu wa Maua Sama, Nyimbo zake Bora, Mahusiano na Thamani Yake

Kazi hii kutoka kwa Maua Sama na Young Lunya inaleta shauku kubwa sana kwa mashabiki kutokana na ukweli kuwa wasanii hao hawajatoa ngoma kwa muda mrefu kidogo.

Mara ya mwisho kwa Maua Sama kuachia wimbo ilikuwa ni miezi saba nyuma alipoachia ‘Wivu’ wimbo ambao alimshirikisha Aslay huku Young Lunya ana miezi takriban minne tangu aachie ngoma yake ya "Mbuzi" mwezi Mei japo siku kadhaa nyuma alifanya freestyle ya wimbo wa Wizkid ‘Essence’.

Bado haijawekwa wazi kama mradi huo ni wa Maua Sama au ni ngoma ya Young Lunya ambaye pia yuko jikoni kuandaa albamu yake ya kwanza tangu aanze muziki.

Leave your comment